Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Sinyamule akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Tanesco Hedaru wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro.
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule  akizungumza na wadau mara baada ya kufungua ofisi ya Tanesco Hedaru.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akiwa katika picha ya pamoja Wafanyakazi wa Tanesco Hedaru.Na Mwandishi Wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule ameigiza Tanesco Same kuwafata wateja popote walipo hili kuongeza kasi ya huduma kwa kuhakikisha kuwa kila mahali wanapata Umeme.

Dc Sinyamule amesema hayo alipokuwa akizindua tawi la Tanesco Hedaru na Kisiwani katika Wilaya Same na kumbusha kuongeza ofisi maeneo ya milimani.

“Kuhakikisha mkandarasi anayefanya kazi kuzingatia uimara wa nguzo hasa maeneo ya milimani pamoja na Kutengeneza mabango yanayoonyesha wateja tahadhari za kuchukua juu ya umeme ili kupunguza madhara ya vifaa na umeme kukatikakatika”Amesema Dc Sinyamule.

Amewataka Kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma kwa haraka na Kuanzisha na kuitangaza namba ya simu ya mkononi kwa ajili ya wateja.

Pia aliwakumbusha wateja kuongeza kasi ya kuweka umeme na kulipia huduma za umeme pindi watakapohitajika kuunganishiwa.

Pia aliwakumbusha kuanza kutumia umeme kwa uchumi kwa kuanzisha viwanda vidogo na vya kati kwani serikali imekusudia kumaliza tatizo la umeme ifakapo 2021.

Kwa Upande wake Meneja wa Tanesco Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Hiza amesema shirika limejipanga kusogeza huduma karibu baada ya ongezeko kubwa la wateja wanaotokana na mpango wa serikali REA.

Hivyo aliwaomba wakazi wa Wilaya ya Same na Vitongoji vyake Kulipa bili kwa wakati na kutumia umeme kwa uangalifu ili kusiwepo umeme unaopotea bila sababu.

Aidha aliwaomba wakazi wa eneo hilo Kuchukua tahadhari za usalama pamoja na kutunza miundombinu na Kutoa taarifa haraka kunapotokea tatizo/uharibifu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: