Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo” wilaya ya Shinyanga ambapo jumla ya wahitimu 238 wamefuzu mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa miezi minne.
Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua gwaride.
Meza kuwa wakiwa wamesimama wakati wahitimu wakipita kwa mwendo wa polepole
Wahitimu wa mafunzo hayo wakipita kwa mwendo wa taratibu/polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wahitimu wa kike wa mafunzo ya jeshi la akiba wakipita mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro
Wahitimu wakitembea kwa mwendo wa polepole
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakipita kwa mwendo wa haraka
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakipita kwa mwenda wa haraka mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkufunzi wa mafunzo ya Jeshi la Akiba na MC wakati wa sherehe hizo,Sajenti Geofrey Kamala akitoa maelekezo
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mhitimu Chacha Warioba akisoma risala
Wahitimu wa mafunzo hayo wakiimba wimbo
Wahitimu wakiimba shairi
Wahitimu wakionesha mchezo wa Singe
Burudani inaendelea
Wahitimu wakionesha mchezo wa ngumi
Wadau mbalimbali wakiwa eneo la tukio
Mshauri wa Mgambo wa wilaya ya Shinyanga Meja Ford Mwakasege akitoa taarifa kuhusu mafunzo ya jeshi la akiba
Mshauri wa Mgambo wa wilaya ya Shinyanga Meja Ford Mwakasege akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga mafunzo mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo”.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo”
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na wakufunzi wa mafunzo hayo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Sherehe za kufunga mafunzo hayo zimefanyika leo Jumatatu Oktoba 9,2017 katika viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga.
Akizungumza katika sherehe hizo,Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia vyema mafunzo waliyoyapata huku akiwaasa kufanya shughuli za maendeleo ili kujiinua kiuchumi.
Matiro aliwataka wahitimu hao kuunda vikundi vya ujasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia.
“Mmejifunza mambo mengi,naomba muzingatie mlichojifunza,muwe wazalendo wa nchi yetu,kuweni mstari wa mbele kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kuwafichua wahalifu na wale wote wanaoleta uvunjifu wa amani katika jamii”,aliongeza Matiro.
Katika hatua nyingine alizitaka kampuni za ulinzi kutumia walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo.
Naye Mshauri wa Mgambo wa wilaya ya Shinyanga Meja Ford Mwakasege alisema washiriki wa mafunzo hayo mwaka huu wengi wametoka katika makampuni ya ulinzi.
“Mafunzo haya yameanza Juni 5,2017 washiriki wakiwa ni 303 lakini leo wamehitimu 238 kati yao wanaume ni 193,wanawake ni 45,na yalikuwa yanaendeshwa na wanajeshi na wanajeshi wa kujitolea,wahitimu pia walishiriki zoezi la upandaji miti lililozinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga hivi karibuni”,alieleza Mwakasege.
Aidha alisema miongoni mwa changamoto zilizopo ni ukosefu wa sare za jeshi la akiba na utoro kwa washiriki hali inayofanya wengi kutomaliza mafunzo.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo,Chacha Warioba alisema miongoni mwa mambo waliyojifunza kuwa ni pamoja na matumizi ya silaha mbalimbali,kwata,rushwa,usalama wa taifa na zimamoto na uokoaji.
Hata hivyo alisema changamoto kubwa kwao ni ukosefu wa ajira hivyo aliiomba serikali iwape kipaumbele katika ajira zinazojitokeza.
Aliitaja changamoto zingine kuwa ni ucheleweshaji wa vyeti vya mafunzo na malipo duni kwenye makampuni wanakoajiriwa hivyo kuiomba serikali kutoa mwongozo wa kima cha chini cha mishahara kwenye makampuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments: