Meneja Utetezi wa Advance Family Planning James Mlala akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya utumiaji vidoge vya uzazi wa mpango duniani. Katikati ni Mwenyekiti wa muungano wa vijana wa kutoa elimu ya afya ya uzazi (Tayari) William Otuck and Mkuregenzi wa Tanzania Communication and Development Centre (TCDD) (TCDC) Deo Ng’wananzabi (kushoto).
Meneja Utetezi wa Advance Family Planning James Mlala akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya utumiaji vidoge vya uzazi wa mpango duniani. Katikati ni Mwenyekiti wa muungano wa vijana wa kutoa elimu ya afya ya uzazi (Tayari) William Otuck.
Mkuregenzi wa Tanzania Communication and Development Centre (TCDD) (TCDC) Deo Ng’wananzabi (kushoto) akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya utumiaji vidoge vya uzazi wa mpango duniani na kulia Meneja Utetezi wa Advance Family Planning James Mlala.
---
Tanzania ni nchi yenye idadi kubwa sana ya vijana; Takribani asilimia 63 ya watu wake milioni 50 wana umri wa chini ya miaka 25. Kundi hili linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na upatikanaji duni wa elimu bora, na huduma za afya ikiwa ni pamoja na Afya ya Uzazi na Ujinsia (SRH), na fursa za kutosha za kazi.
Mimba za utotoni zimeendelea kuongeza watoto wa kike wasiopata fursa ya kukamilisha elimu yao na kupata kazi nzuri. Kwa mujibu wa utafiti wa Afya na idadi ya watu Tanzania (TDHS-MIS) 2015-16 inaonyesha kwamba kiwango cha mimba za utotoni kimepanda kutoka 23% mwaka 2010 hadi 27% mwaka 2015.
Mimba za utotoni huchangia sana kuongezeka kwa vifo vya uzazi na utoaji mimba usio salama nchini.
Miongoni mwa sababu nyingi zinazochangia changamoto hizi, ni pamoja matumizi ya madogo ya njia za uzazi wa mpango kwa vijana, ambapo ni 13% tu. Kwa mujibu wa TDHS, 16% ya wanawake walioolewa sasa wenye umri wa miaka 15-19 na 20% ya wale wenye umri wa miaka 20-24 wanahitaji huduma za uzazi wa mpango lakini hawazipati.
Upatikanaji hafifu wa taarifa na huduma za uzazi wa mpango kwa vijana huchangia kiwango cha juu uzazi ambacho kwa sasa ni watoto sita kwa kila mwanamke wa kitanzania aliye katika umri wa uzazi.
Matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango (mCPR), yameongezeka kutoka 27% mwaka 2010 hadi 32% mwaka 2015. Matumizi ya uzazi wa mpango huchangia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa 44% Tanzania.
Tunapoadhimisha siku ya Njia za Uzazi wa Mpango, sisi Mtandao wa Vijana kuhusu Afya Ya Uzazi (TAYARH Coalition) tunapenda kuipongeza serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya kisera ambayo yamesaidia ongezeko la utekelezaji wa mipango ya Afya ya Uzazi kwa vijana.
Hata hivyo, tunatoa wito kwa serikali, wadau wa maendeleo, mashirika ya kimataifa, sekta binafsi na makampuni kuongeza uwekezaji ili kuhakikisha kuwa vijana wote wanapata taarifa na huduma bora za Afya ya Uzazi na hasa uzazi wa mpango bila unyanyapaa au ubaguzi.
Aidha, tunatoa wito maalum kwa serikali kuharakisha utekelezaji wa lengo lake la kuongeza idadi ya vituo vya kutoa huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana kutoka 30% mwaka 2015 hadi 80% kama ilivyoelezwa katika mkakati wa pili wa kuharakisha kupunguza vifo vya mwanawake na watoto Tanzania uitwao One Plan II (RMNCAH 2016-2020) na ni moja ya maazimio ya taifa kwenye mpango wa kimataifa uitwao FP2020 uliotangazwa upya mjini London mwezi Julai 2017.
Tunapenda kuisihi serikali kupitisha mtaala wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia mashuleni ili kujenga ufahamu wa vijana kuhusu njia ya kuepuka kuanza masuala ya ngono katika umri mdogo.
Tunatambua uwepo wa kanuni za kidini, kijamii na kitamaduni, lakini hali halisi ya sasa inayochangia unyanyasaji wa kijinsia kwa vijana, inahitaji mbinu tofauti ili kukabiliana na changamoto hizo.
Kwa upande mwingine, TAYARH inawasihi vijana wote nchini kutafuta kikamilifu taarifa na huduma za Afya ya Uzazi, kuwa na shauku ya kujihusisha katika masuala ya kisera na utoaji wa maamuzi ili kuhakikisha kuwa watoa maamuzi kuhusu huduma hizi wanawajibika ipasavyo. Na pia kuhamasisha vijana wenzao kuhusiana na masuala haya.
Kutokujali afya ya uzazi kwa vijana hakutakuwa na athari kwa ustawi wa jamii tu, bali pia kiuchumi. Lakini pia jitihada za Tanzania za kujenga uchumi wa kipato kati ifikapo mwaka wa 2025 kutaendelea kukabiliana na changamoto zaidi. Kwa sasa, kila mtu mzima anayeingiza kipato anategemeza wastani wa watu tisa. Uwezo wa watu binafsi na familia kuweka akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye pia kunaathiriwa na changamoto hizi.
TAYARH inatambua kuwa kwa Tanzania kunufaika na muundo wa idadi ya watu wake kiuchumi, ni muhimu iongeze jitihada za kupunguza kasi ya uzazi kwa watu wake, na uwekezaji zaidi uelekezwe katika kuboresha afya, elimu, mageuzi ya kiuchumi, kuongeza fursa za ajira na kuimarisha utawala bora katika ngazi zote za uongozi. Vijana ni wadau muhimu katika juhudi hizi, hivyo sisi sote tunapaswa kuwajibika kikamilifu ili kujenga mustakabali bora wa baadaye na matumaini kwetu na ya watoto wetu.
TAYARH inaendelea kuhusisha na kuhamasisha Asasi Za Kiraia (AZAKI) zinazoongozwa na vijana ili kuimarisha uwezo wao katika masuala ya afya ya uzazi, kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya ya uzazi hasa matumizi ya njia za uzazi wa mpango, na kuwawajibisha viongozi kuhusu maazimo na ahadi za kitaifa na za kimataifa ili kuboresha upatikanaji huduma na taarifa sahihi kwa vijana.
Toa Maoni Yako:
0 comments: