Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto,Bi Sihaba Nkinga akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa watoto
ulioandaliwa na taasisi ya REPSSI yenye makao yake nchini Afrika Kusini kutoka mataifa zaidi ya 30 barani Afrika unaofanyika jijini Arusha, mkutano huo pamoja na mambo mengine unalenga kuwawezesha watoto sauti zao kusikika na kuwajenga kisaikolojia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya REPSSI, Noreen Huni ambaye ni raia wa Zimbabwe akizungumza katika mkutano huo wa kimataifa jijini Arusha leo.
Watoto kutoka mataifa mbalimbali wakifatilia mada kwenye mkutano huo.
Watoto kutoka mataifa mbalimbali wakiwa kwenye mkutano ambao unawapa fursa ya kuwasilisha taarifa za matukio ambayo ni changamoto kwao.
Watoto wakiwa kwenye mkutano ambao unawapa fursa ya kuwasilisha taarifa za matukio ambayo ni
changamoto kwa mamlaka husika na kutafutiwa ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia,Wanawake na Watoto, Bi Sihaba Nkinga(katikati) akiwa katika  picha ya pamoja na Mwenyekiti wa baraza la watoto nchini,Joel  Festo (kushoto) na Mwenyekiti wa baraza la watoto nchini Kenya,Brian Musyoka katika  mkutano wa kimataifa wa watoto ulioandaliwa na taasisi ya REPSSI yenye  makao yake nchini Afrika Kusini.
Mmoja wa washiriki akifatilia kwa makini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto, Bi Sihaba Nkinga (katikati) akiagana na  viongozi wa watoto mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Arusha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: