Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Rev. Flaston Ndabila, akitoa mahubiri  katika ibada  maalumu ya kuwasimika wachungaji watano na kuwawekea wakfu wengine watano kuwa waangalizi wa kanisa  hilo katika ibada iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
 Mwangalizi  wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka  America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja akiwasalimia waumini wa kanisa hilo. Mchungaji Agbeja aliongoza ibada hiyo. Kulia ni Mtumishi wa Mungu, Zephaniah Andrew Nyambele ambaye alikuwa ni Mkalimali katika ibada hiyo. 

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ibada hiyo akizungumza kwa niaba ya serikali.
 Wachungaji waliosimikwa. Kutoka kushoto ni  Ezekiel Katani kutoka Mbeya, Mbarikiwa Mwakatika kutoka Morogoro na  Leonard Mandia, Cosmas Nchimbi Morogoro na Joel Nsalila kutoka Dar es Salaam.
 Wachungaji waliowekwa wakfu kuwa waangalizi wa kanisa hilo katika majimbo. Kutoka kushoto ni Prince Twahir Rubeya, George Ntara,, John Muhembano, Lois Malali na Nathaniel Ndabila kutoka Mbeya na wengine waliobaki wanatoka Dar es Salaam.
 Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Kwaya ikiimba nyimbo za kusifu.
 Maombi yakifanyika.
 Ibada ikiendelea.
 Wachungaji wakisimikwa. Katikati kushoto ni Mwangalizi  wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka  America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja akiwasimika wachungaji hao. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Rev. Flaston Ndabila.
 Wachungaji hao wakisimikwa.
 Ibada ya kuwasimika ikiendelea.
 Mwangalizi  wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka  America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja akiwapaka mafuta wachungaji hao.
 Mwangalizi  wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka  America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja, akiwaombea wachungaji hao wakati wa kuwasimika. Wa pili kushoto ni Mama Askofu  Rev. Flaston Ndabila na wachungaji wengine wakishiriki kuwaombea wachungaji hao.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC),  Rev. Flaston Ndabila, akiwaombea wachungaji hao waliosimikwa.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC),  Rev. Flaston Ndabila, akiwapongeza wachungaji hao.
 Wachungaji wakiwekwa wakfu kuwa waangalizi wa kanisa hilo.
  Mwangalizi  wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka  America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja, akimpaka mafuta Mchungaji, Lois Malali kuwa mwangalizi wa kanisa hilo.
 Wachungaji hao wakiombewa na wachungaji wenzao.
 Maombi yakiendelea.
 Maombi yakifanyika.
 Wake wa wachungaji hao wakiwa katika maombi.
 Wachungaji hao uso kwa uso na wake zao katika ibada hiyo.

Na Dotto Mwaibale

VIONGOZI wa Dini wametakiwa kuwa mstari wa mbele kwa kuyaunganisha makundi yote yaliyopo kwenye makanisa yao ili kuliletea taifa la Tanzania maendeleo badala ya kuyagawa. 

Ombi hilo limetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC),  Rev. Flaston Ndabila wakati akihubiri  katika ibada  maalumu ya kuwasimika wachungaji watano na kuwawekea wakufu wengine watano kuwa waangalizi wa kanisa  hilo katika ibada iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

"Kazi kubwa mlionayo ninyi wachungaji mliosimikwa leo hii ni kwenda kuwatumikia watanzania na makundi mengine yote yaliyopo katika makanisa yenu badala ya kuyagawa" alisema Rev. Ndabila.

Rev. Ndabila aliyataja makundi hayo yaliyopo makanisa kuwa ni wanasheria, wataalamu, wanasiasa, wajane watoto na yale yenye uhitaji maalumu ambapo aliwata wachungaji hao kwenda kuwatumikia na kuwaunganisha bila kujali itikadi zao kwani kanisa halina ubaguzi.

Alisema ndani ya makundi hayo wapo watu wanahitaji faraja hivyo waende wakawape faraja badala ya kuwatenga kwani faraja watakayopata itawasaidia wasonga mbele kiimani na kimaendeleo. 

Alisema Tanzania inataka kiongozi atakayekuwa anawaunganisha wananchi bila kujali mtu huyo anatoka kundi gani na ana itikadi gani lengo likiwa ni kuleta maendeleo ya nchi.

Aliongeza kuwa kiongozi anayetakiwa ni yule atakaye saidia watanzania kupata ufahamu wa kujua utajiri uliopo nchini na rasilimali zilizopo na jinsi zitakavyo wanufaisha na kuondoa dhana ya kuwa nchi yetu ni maskini licha ya kuwa ni tajiri.

Katika hatua nyingine Askofu Ndabila aliwataka wananchi kujenga tabia ya kuthamini juhudi mbalimbali za kuliletea taifa maendeleo zinazofanywa na viongozi akiwemo Rais wetu Dk. John Magufuli ili kuwatia moyo badala ya kuwabeza.

"Viongozi wetu wanafanya juhudi mbalimbali za kuijenga nchi ni vizuri wote kwa pamoja tukawatia moyo badala ya kuwabeza" alisema Ndabila.

Askofu Ndabila aliwataka wachungaji hao kwenda kuwatumikia wananchi kupitia kanisa badala ya kutumia madhabahu kwa ajili ya kujitajirisha na kuwa wabinafsi ambapo pia aliwaonya kuacha kutumia lugha isiyoeleweka kwa waumini wao badala yake watumie lugha nyepesi wanayoifahamu kama lugha ya taifa jambo litakalosaidia kuondoa mikanganyo wanapotoa mahubiri.

Mwangalizi  wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka  America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja alisema ,Tanzania ni nchi ya amani na iliyojaa neema ambapo amewaomba watanzania waendelee kuitunza.

“Nawaomba watanzania tunzeni amani mliyonayo ,nimetembea nchi nyingi lakini nimeona kuwa Tanzania ni moja ya nchi yenye amani watu katika makanisa wana abudu kwa furaha kutokana na amani iliyopo hivyo hamna budi kuitunza amani hii" alisema Dk. Omolayo.

Dk. Omolayo alisema alishangaa watu wakiuza matunda mengi ambayo ni mazuri mitaani tofauti na nchi nyingine hali ambayo inatokana na nchi iliyobarikiwa kwa kuwa na ardhi yenye rutuba.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ibada hiyo kwa niaba ya serikali, Asumpter Mshama aliwataka waumini wa dini zote wasiwe watu wa kutoa lawama kwa serikali kuwa haifanyi chochote bali waisaidie serikali ili kuiletea nchi maendeleo kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Dk.John Magufuli.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: