Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete,akionyesha Kilimo cha mahindi ya njano kwa ajili ya kuongeza rutuba kwa ng'ombe .
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt.Jakaya Kikwete,akionyesha eneo analohifadhi majani ya malisho ng'ombe .
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete,akionyesha baadhi ya mifugo yake na kueleza umuhimu wa Ufugaji wa kisasa ili kupata maziwa ya kutosha na ng'ombe kuwa na afya.(Picha na Mwamvua Mwinyi).

Na Mwamvua Mwinyi, Msoga.

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt.Jakaya Kikwete ,amesema ameanza kufanya kilimo na ufugaji tangu mwaka 1988/1989 hivyo anaetegemea kufanya shughuli hizo baada ya ustaafu amechelea .

Aidha ameeleza matarajio yake kwa sasa ni kuongeza mifugo ya ng'ombe majike wa maziwa 500 watakaoweza kutoa maziwa lita 2,000 hadi 4,000 kwa siku .

Katika hatua nyingine dk.Kikwete amesema endapo wafugaji watazingati ufugaji wa kisasa kwa kuwa na maji ya kutosha ,malisho ,kinga ya chanjo na kuogeshwa ni lazima watanufaika kwa kupata soko la uhakika hasa maziwa .

Akizungumza baada ya kutembelewa na baadhi ya waandishi wa habari mkoani Pwani ,shambani kwake Msoga ,Kikwete alisema anaetarajia kufuga na kulima akifika miaka 67 atapata changamoto kwani sio kazi rahisi.

"Ukishazeeka ndio uanze kufuga ama kulima ,ahaahha haahah (alicheka) itakuwa ngumu sana ,kwani pia hata miaka ya kuishi hatujui " alisema dk.Kikwete .

Alifafanua endapo atafikia malengo aliyojiwekea ataweza kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza siagi.

Alisema kwasasa anang'ombe zaidi ya 400 mchanganyiko ambapo 46 ndio wanakamuliwa maziwa na kutoa lita 400 kwa siku na hununuliwa yote .

Alieleza maziwa yana soko kama utamtunza ng'ombe hivyo kutokana na ufugaji anaoufanya anauhakika atafikia adhma yake .

Alielezea kuwa,kwa kufuata ufugaji wa kitaalamu amelima hekari 30 za mahindi ya njano kati ya hekari 800 alizonazo ambayo husaidia virutubisho kwa ng'ombe ambapo wameshavuna hekari nne na wanaendelea kuvuna.

Dkt. Kikwete alisema, anatarajia pia kulima majani ya malisho zaidi hekari 200 zaidi ili zitosheleze mahitaji.

"Nilianza kufuga ng'ombe 20 kule Bagamoyo wakati nikiwa waziri baadae nikawahamishia Msoga na wameendelea kuongezeka " alisema Dkt. Kikwete.

Alibainisha ,miaka miwili iliyopita wafugaji hususan wa Msoga walipata hasara ya mifugo yao kufa kwa wingi kutokana na ukame .

Dkt.Kikwete alisema yeye alibahatika ,hakuna hata mfugo wake uliokufa kutokana na akiba aliyojiwekea ya malisho na maji .

Kuhusu kilimo cha mananasi alisema alianza mwaka 1989 .

"Mananasi huvunwa baada ya miezi 18 tangu kupandwa"

Dkt. Kikwete alisema shamba lake lina ukubwa wa hekari 200 ambapo hekar 64 ndizo zimelimwa .

Alisema wakulima wa mananasi wana changamoto ya maji ya umwagiliaji ,wakipata maji wataweza kuvuna wakati wowote .

Mstaafu huyo alisema wanahitaji dola mil.15 katika mradi wa maji ya umwagiliaji kwani maji yapo mbali WAMI.

Alisema ametumia umaarufu wake na kuweka mitego yote lakini bado hajafanikiwa ila ipo siku watafanikiwa kupata mradi huo .

Baadhi ya wakazi waliopata kibarua cha kuvuna mahindi ya njano kwenye shamba la dk.Kikwete wamemshukuru kwa kuwapatia ajira .

Walisema wameweza kujiendesha na maisha yao ya nyumbani ikiwemo watafutia watoto wao mahitaji ya kielimu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: