Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa

Meneja Pensheni wa PSPF, Bw. Mohammed Salim, akitoa mada juu ya maandalizi na fursa za wastaafu

Afisa Mwandamizi wa Utafiti wa PSPF, Bw. Mapesi Maagi, akigawa vitendea kazi kwa washiriki wa semina mwanzoni mwa mafunzo hayo

Bw. Silayo, (Kushoto), akiteta jambo na Meenja wa Mipango na Utafiti wa PSPF, Bw. Luseshele Njeje.

Mshiriki akizunguzma wakati wa semina hiyo

Afisa Uhusino Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akitoa utaratibu wa namna semina hiyo itakavyoendeshwa

Mshiriki akinukuu kilichokuwa kikiendelea

Wanasemina wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa

Baadhi ya wadau wa PSPF, na washiriki wa semina wakifuatilia mada zilziokuwa zikitolewa

Washiriki wa semina wakiwa kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo BoT jijini Mwanza

Bw. Silayo, (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Meneja wa Fedha wa Mfuko huo, Bw.Lihami Masoli

Kuonyesha semina hiyo ilikuwa muhimu kwa wastaafu hawa watarajiwa, mshiriki wa semina akinakili kwa uangalifu mkubwa yaliyokuwa yakielezwa (mafunzo).

Afisa Mfawidhi wa PSPF, mkoani Mwanza, Bw.Salim Salum, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo na katikati ni Meenja wa Pensheni wa Mfuko huo, Bw. Mohammed Salim

Sehemu ya washiriki wa semina

Mshiriki akipitia ratiba.

Washiriki hawa wakipitia vipeperushi vya PSPF vyenye taarifa mbalimbali za Mfuko.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MAKAMU wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa
kufungua rasmi semina kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na
Mfuko
wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo kwa
watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), jijini Mwanza.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, kwenye ufunguzi wa semina hiyo
iliyoanza leo Juni 2, 2017, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw.
Gabriel Silayo alisema, semina hiyo inalenga kuwandaa kwa kuwapa mafunzo
watumishi wa umma ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni, ili
hatimaye wastaafu kwa amani.
“Na kwa kufanikisha hilo,
tunao maafisa wetu watatoa mada mbalimbali, wapo washirika wetu, SIDO,
na mabenki kama vile NMB, CRDB, TPB, MCB na UTT, ambao watatoa elimu ya
namna bora ya kutunza na kutumia fedha zako za mafao.” Alibainisha Bw.
Silayo.
Bw. Silayo pia alisema, kwa kutambua kipaumbele
cha serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake, Rais Dkt. John
Pombe Magufuli, kauli mbiu ya semina hiyo ni “Mafao ni Mtaji wa
Uwekezaji Sahihi”. “Na ndio maana tumewaleta SIDO hapa ili wawaelimishe
jinsi mtakavyoweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo baada ya kustaafu
utumishi wa umma na ndugu zangu napenda niwahakikishie hilo
linawezekana.” Alisema
Alisema semina hiyo itakuwa ya
siku mbili na kwamba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mama Samia Suluhu Hassan ataifungua rasmi kesho Jumamosi Juni 2, 2017.
Zaidi
ya watumishi 300 kutoka sekta mbalimbali za utumishi wa umma kwenye
wilaya zote za mkoa wa Mwanza wanahudhuria semina hiyo ya mafunzo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: