Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akiwasilisha makadirio
ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapo aliliomba Bunge liidhinishe
Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la
Bajeti,mjini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akijibu maswali
yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali
yaliyoulizwa na Wabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kulia ni
Naibu Waziri wa wizara hiyo,Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu
maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali
yaliyoulizwa na Wabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kushoto
ni Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Projest
Rwegasira, akizungumza na makamanda wa Jeshi la Polisi muda mfupi kabla
ya kuanza kwa kikao cha Bunge la Bajeti ambapo wizara yake iliomba Bunge
liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000.Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akifurahia na baadhi ya wabunge mara baada ya kumaliza kuwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapo aliliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.


Toa Maoni Yako:
0 comments: