Mwanasheria wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC) Abia Richard, akizungumza wakati wa Tamasha la Vijana la kupinga Ukatili wa Kijinsia lililofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Picha Zote na Nasma Mafoto.
Wachezaji wa timu za Simba Queens na Mburahati Queens, wakichuana kuwani mpira wakati wa mchezo wao kwenye Bonanza hilo. Katika mchezo huo Mburahati Queens, waliibuka washindi kwa mikwaju ya penati 4-2. Picha Zote na Nasma Mafoto
Viongozi wakikagua timu kabla ya kuanza kwa mtanange wa Soka kwa upande wa wanaume.
Kikosi cha Simba Queens
Kikosi cha Mburahati Queens.
Na Karama Kenyunko
Kituo cha
Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC), kimeanzisha bonanza maalum la
michezo kwa ajili ya kuhamasisha jamii kupinga ukatili wa kijinsia.
Bonanza hilo, limefunguliwa na mratibu wa WLAC, Abia Richard jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo uliofanyika Mwembe Yanga,Temek, Abia
amesema lengo la kuanzishwakwa bonanza hilo ni kutaka kuwaunganisha
watanzania kupambana na vitendo hivyo bya ukatili wa kijinsia.
Amesema,
katika kampeni nyingine ambazo wamekuwa wakiendesha, kundi kubwa ambalo
limekuwa likihamasika ni wanawake na wasichana kwa hiyo wanaamini
kuanzisha kampeni hiyo kutasaidia kuwahamasisha na wanaume.
Ameongeza,
kati ya kundi linalotajwa katika kutenda vitendo vya ukatili wa
kijinsia na wanaume pia wamo, lakini katika kampeni nyingi
zinazoendeshwa za kuhamasisha kupambana na vitendo hivi, kundi la
wanaume wamekuwa wakijiweka pembeni.
" Tunaamini katika kampeni hii kupitia bonanza, wanaume watashiriki kwa wingi kwa sababu wanapenda michezo,” amesema Abia.
Ameongeza
kuwa, vitendo vya ukatili wa kijinsia vinapaswa kupambanwa na kila mtu
katika jamii kwa kuwa vinaathiri sana jamii yetu. Wanaume hawapaswi
kukaa pembeni, tunawaomba kupitia michezo hii nao washiriki kupambana
navyo.
Katika kampeni hiyo michezo mbalimbali
imepangwa, kuwamp ikiwemo ya mpira wa miguu, pete, na mingine mingi,
itakayowapa fursa na wanaume kushiriki.
Pia alisema
wanatarajia kuanzisha timu baina ya madereva wa boda boda, bajaji na za
vijana kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwahamasisha kuelimisha
jamii kupinga vitendo hivyo.
Katika uzinduzi wa kampeni
hiyo, timu ya mpira ya wanawake ya Simba gueen na Mburahati queen zote
za jijini Dar es Salaam, zilimenyana na kutoka sare ya bila kufungana.
Toa Maoni Yako:
0 comments: