Mwandishi Wetu

Katika hali ya kukabaliana na mabadiliko ya mahitaji ya wateja, Tigo imeendelea kubuni bidhaa na huduma kwa wateja wenye biashara zinazosadifu sehemu tofauti ndani ya soko la Tanzania.

Huduma hizo za Tigo kwa ajili ya makampuni na biashara mbalimbali zinajumuisha aina tofauti za huduma za mawasiliano kwa simu (voice), SMS, pamoja na vifurushi vya data.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni jijini Dar es Salaam Afisa Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo, Hussein Sayed alisema kuwa huduma hizi ni kwa ajili ya wamiliki wa makampuni na biashara ambao wako makini kuhusu suala la gharama. Vile vile huduma hii inatoa viwango vya ushindani hadi kufikia asilimia 70 ya viwango vilivyopo katika soko.

“Licha ya kufurahia viwango bora zaidi katika soko na usimamizi wa hali ya juu wa akaunti, wateja wanawezeshwa kukamilisha biashara zao kwa kutumia mtandao mkubwa na wenye kasi ya intaneti ya 4G LTE ulioenea katika miji 22 ya Tanzania wakati huo huo wakifurahia vifurushi vya data vya Tigo,” alisema Sayed na kuongeza kuwa wateja watapata kifurushi mara mbili kila wanaponunua kifurushi cha data cha zaidi ya shilingi 25,000 ambayo ni promosheni tuliyo nayo kwa muda sasa.

“Kama nyongeza wateja wapya watakuwa wanafurahia kupata data za bure ikiwa ni ofa iliyozinduliwa na Tigo katika kuwaunga mkono wafanya biashara wa Tanzania katika uendeshaji wa shughuli zao za kila siku,” alisema Sayed.

Akizungumzia huduma za kampuni hiyo ya simu; Sayed alisema kuwa zimeundwa kwa umakini hivyo kwamba huduma zote zitawapatia wateja thamani zaidi na wakati huo huo zikiwasaidia kupunguza gharama za mawasiliano.

Aliongeza, “Kuunganishwa na mawasiliano ni jambo muhimu katika kufanikisha miamala ya kibiashara kwa karne hii ya 21; na ndio maana tupo makini katika kubuni huduma/bidhaa mbalimbali zinazokidhi mahitaji ya biashara kubwa,za kati na ndogondogo katika soko la Tanzania.”

Sayed alisema kuwa mafanikio ya Tigo katika utoaji wa huduma zinazolenga biashara nchini kumechangiwa na kampuni kufanya uwekezaji mkubwa katika vifaa ndani ya kituo cha kutunza kumbukumbu (Data centre), teknolojia za huduma kwa intaneti na kuwapa mafunzo ya uhakika wafanyakazi na kuwajengea uwezo ambao wamekuwa wakiwapatia wateja suluhisho zuri katika mahitaji yao ya kibiashara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: