Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt. Workneh Gabeyehu wakisaini mkataba unaolenga ushirikiano katika kupambana na uhamiaji haramu, masuala ya biashara na mapambano na ugonjwa wa malaria
Ikulu Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia Dkt. Hirut Teketel wakisaini mkataba wa makubaliano yanayotoa fursa za uwekezaji pamoja na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utalii Ikulu Jijini Dar es salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia Dkt. Hirut Teketel wakibadilishana mikataba wa makubaliano yanayotoa fursa za uwekezaji pamoja na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utalii Ikulu Jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn akiongea na waandishi wa habari katika hafla ya utiliaji saini mikataba ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia ambao amemuahidi kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali za maendeleo, Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ikulu leo Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn ikulu leo Jijini Dar es Salaam. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: