Kampeini ya Taifa Moja inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii kwa matamasha ambayo yatafanyika kwenye mikoa mitano hapa nchini ikiwa na lengo ya kuendelea kutoa burundani pamoja elimu kwa Watanzania juu ya kutuma na kupokea fedha kutoka kwenye mtandao wowote kwa gharama ile ile.

Taifa Moja ni kampeni ambayo imedhaminiwa na taasisi za Financial Sector Deepening Trust of Tanzania (FSDT) pamoja na Bill & Melinda Gates Foundation huku ikiratibiwa na International Finance Corporation (IFC) chini ya muungano ya makampuni matatu ya simu za mkononi za Airtel Tanzania, Tigo Tanzania na Zantel kupitia huduma zao za Airtel Money, Tigo Pesa na Ezy Pesa.

Akizungumza jijini leo Jijini Dar es Salaam, Liginiku Milinga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Fern Tanzania ambao ndio waratibu na waandaaji wa matamasha hayo alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata burundani toka kwa wasanii wakali hapa nchini na pia kupata elimu juu ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote hapa Tanzania kwa gharama ile ile.

Milinga alitajwa mikoa ambayo matamasha hayo yatafanyika ni pamoja na Mbeya (Mwenge Primary School), Dar es Salaam (Zakhiem Grounds), Arusha (Kilombero Grounds), Mwanza (Furahisha Grounds na Tabora (Uyui Grounds) huku msanii Chege akitumbuiza Mwanza, Stamina na Jambo Squad wakitumbuiza Arusha, Belle 9 Mbeya, Cassim Mganga Tabora huku Mkubwa na wanae wakifanya yao Jijini Dar es Salaam. Matamasha hayo yatafanyika Jumapili ya tarehe 16 April mwaka huu. 

Kuhusu kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao kwa gharama ile ile Meneja Chapa kutoka kampuni ya Tigo Tanzania William Mpinga, Moses Alphonce ambaye ni Meneja wa Airtel Money, Patric Dumulinyi ambaye ni Mobile Money Manager walitoa wito kwa wananchi kwenye mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwani matamasha haya ni ya wazi na hakuna kiingilio.

‘Natoa wito kwa Watanzania kujitokeza na kupata elimu ya kutosha ya jinsi ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote kwa gharama ile ile, alisema,’ alisema Mpinga.

Mpinga alisema huduma hiyo itawanufaisha wananchi kupunguza gharama za kutuma fedha kwenda mitandao mingine na upotevu wa fedha uliokuwa ukijitokeza hapo awali.

Alisema kampeni ya Taifa Moja itaongeza uelewa wa watumiaji wa simu za mikononi nchini juu ya namna ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine kwa gharama ile ile.

“Watumiaji wa huduma za simu-pesa watatumiana pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine na kuingia moja kwa moja kwenye akaunti za simu –pesa ya mteja aliyetumiwa, hakutakuwa na sababu ya kuhofia pesa hiyo uliyotumiwa kwenda kuitoa haraka ukihofia kumrudia aliyekutumia kama ilivyokuwa hapo awali," aliongeza Moses Alphonce kutoka Airtel Money.

Kwa upande wake, Rukia Mtingwa ambaye ni Meneja Chapa na Mawasiliano alisema njia hii ya sasa ni tofauti na utaratibu wa zamani ambao mteja akimtumia mwenzake ambaye yupo mtandao mwingine hutumiwa ujumbe wa meneno (sms) kwa aliyetumiwa kwenda kuchukua pesa hiyo kwa wakala.

“Kuanzia sasa tutaendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa mitandao yetu juu ya utumaji pesa kutoka kwenye mtandao mmoja kwenda mwingine anavyoweza kukatwa kiasi cha fedha kile kile kama ambacho angelikatwa kutoka mtandao kama wake.”Aliongeza Mtingwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: