Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MCHEZO wa bahati nasibu unaoendeshwa na Biko, unaotambulika kama Ijue nguvu ya Buku unatarajiwa kuchezesha droo yake ya kwanza ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, Jumapili hii.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe (wapili kushoto), akimkabidhi Leseni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BIKO Charles Mgeta kwa ajili ya kufanya shughuli za mchezo wa kubahatisha nchini. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Udhibiti wa Bodi hiyo Sadick Elimusu na Kulia ni Meneja Masoko wa BIKO Goodhop Heaven. Picha zote na Mpigapicha Wetu.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BIKO Charles Mgeta mara baada ya kupeana leseni ya kufanya shughuli za mchezo wa kubahatisha nchini unaoitwa kama Nguvu ya Buku. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Biko, Charles Mgeta, alipofanya mazungumzo na waandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Akizungumza katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mkuu Mgeta, alisema droo yao itakuwa ya kwanza tangu walipoanzisha mchezo huo wenye zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10000, 20000, 50,000, 200,000 na sh Milioni moja, huku zawadi ya Sh Milioni 10 ikipatikana kila mwisho wa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Biko, Charles Mgeta wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea leseni ya uendeshaji wa michezo ya kubahatisha kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe wa pili kushoto. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Udhibiti wa Bodi hiyo Sadick Elimusu na Kulia ni Meneja Masoko wa BIKO Goodhop Heaven.
Charles Mgeta akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari juu ya kampuni yao ya Biko kuendesha michezo ya kubahatisha, ambapo Jumapili hii watachezesha droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kuipa leseni kampuni ya Biko inayondesha mchezo wa kubahatisha unaojulikana kama Nguvu ya Buku.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Biko, Goodhope Heaven, kulia akizungumza na waandishi juu ya mchezo wao wa kubahatisha unaojulikana kama Nguvu ya Buku, ambapo mwishoni mwa wiki hii watachezesha droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10.

“Leo pamoja na kutangaza juu ya kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 Jumapili, bali pia tumekabidhiwa rasmi cheti cha utendaji wa kazi zetu kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, ambapo tunaamini safari yetu itakuwa ya mafanikio zaidi kwa Watanzania.

“Taratibu zetu ni rahisi kwa sababu washiriki wetu wanatakiwa kufanya miamala ya simu za MPESA, TIGO PESA na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni yetu ambayo ni 505050, huku pia akipaswa kuingiza namba ya kumbukumbuku ambayo ni 2456 ambapo kila ujumbe mmoja wa simu atatozwa kwa sh 1000, huku kiasi hicho cha pesa kikiwa na nafasi mbili ikiwa ni zawadi za papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kumuingiza kwenye droo ya wiki ya kujishindia Sh Milioni 10,” Alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe, aliwapongeza BIKO kwa kuingia katika mchezo huo kama sehemu ya kuwapatia maisha bora Watanzania kwa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha.

“Naomba kuwatangazia Watanzania kwamba BIKO wamesajiliwa rasmi katika kuchezesha michezo hii na tunawaambia kwamba wapo salama hivyo kila Mtanzania apaswa kucheza ili aweze kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi wa zawadi mbalimbali,” Alisema Mbalwe.

Biko wameanza kuchezesha mchezo huo wa bahati nasibu huku wakiwa wamejiwekea malengo makubwa ya kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anajiwekea fursa ya kuibuka na ushindi wa zawadi mbalimbali kwa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha kutoka kwenye kampuni yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

4 comments:

  1. Mimi kwasasa nashindwa wa elewa siku ya jana tar19 oct mlini rushia sms kwenye namaba yangu ya tigo ambayo nimecheza nayo sna huu mchezo na nime tumia garama nyingi ila sion kitu naona tuu sms za washindi toka dsm ila mikoa mingine sijaona ila jana mka ni sms kua mwatoa laki laki je anzia saa tatu usiku mpka saa sita nikacheza kwash elf10 ila ata sms ya mshnd ata mmja sijaona pilinina kete takriban 30 ila sishindi wala sipew ratiba kamili tafadhalin tuna waamin hivyo bas ili kuwe na mafanikio mazuri kwenye mchezo huu kusiwe na upendeleo wowote maana kila mtu ni mtaftaji apa

    ReplyDelete
  2. Tafadhalini ningependa kuwa asa sana muwe makini sio hela ya mtanzania wa dar es saalam tuu ina thamani maana watu mna tushawishi tuna cheza tena sana kwa gharama kubwa na hakika alafu washindi wote hutoka dsm je nikwel hakuna watu wamikoa tofauti tumecheza sana lakini ata taarifa zinazazo eleweka hatupew embu kama ni bahati na sibu isi egeemee tuu kwa dar es salaam maana kila mikoa mwatangaza na tunacheza. Jana saa tatu usiku mmetuma sms kua cheza sasa kbla ya sita usiku laki laki ziko nje watu tume cheza ila hata walo shinda mdahuo majina hatuja yaona. Naomben mchezo uwe wa haki kwa kila mtu maana sasa kila kona watu wana tilia shaka huu mchezo sio mimi tu.

    ReplyDelete
  3. Mbona nmefanya muhamala
    Yaani nmecheza alaf hakuna message yeyote iliyoingia ixpokuwa ya tigopesa.. Tu

    ReplyDelete
  4. In kweli washindi no was DSM tu, wawe wakweli nakama mikoani hatumo tunashiriki tu kwa niaba ya kutunisha mfuko, apana wawe wazi wasiwe wezi,

    ReplyDelete