Mbunge wa mstaafu wa jimbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Philemon Ndesamburo akikabidhi kadi
pamoja na pikipiki kwa Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa
Kilimanjaro (Mecki).Nakajumo James. Ndesamburo ametoa msaada wa pikipiki
hiyo kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi wa klabu hiyo.
Katibu wa chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro (Mecki) Nakajumo James akijaribu pikipiki iliyotolewa na Ndesamburo kwa ajili ya shughuli za klabu
Na Dixon Busagaga,
MBUNGE mstaafu wa jimbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo leo amekabidhi pikipiki aina ya Fekon kwa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro. (Mecki).
Msaada huo wa pikipiki ni sehemu ya ahadi za Ndesamburo aliyowahi itoa hapo awali ili kukisaidia chama hicho na changamoto za usafiri.
Akizungumza wakati wa tukio la makabidhiano hayo lililofanyika katika hoteli ya Keys Ndesamburo amesema anathamini mchango wa wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro ambao wametoa na wanaendelea kutoa kwa jamii hali iliyochangia kuwepo kwa utulivu katika mkoa huo.
Katibu wa chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro (Mecki) Nakajumo James ametoa shukrani kwa niaba ya wanachama wa MECKI kwa msaada huo na kwamba kwa sasa mipango inaandaliwa ili iweze kutumika kama bodaboda.
"Kilichopo sasa mbali na kubadili jina la kadi litamburike kwa jina la Mecki pia atatafutwa mtu wa kuitumia kama bodaboda alete mapato kila siku, matarajio ni aidha mtu huyo awe mwandishi kama atamudu kuleta hesabu au mtu mwingine ambaye ataaminika na hili litafanyika kupitia vikao vya chama"alisema James.
Alisema pikipiki hiyo inatarajia kutumika kwa maslahi ya klabu na si vinginevyo na kwamba lengo ni kuleta faida na kuongeza idadi ya pikipiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments: