Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiogozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo wakati alipopokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017. Kulia ni mkewe Mary.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili nchini Mauritius leo (Jumapili, Machi 19, 2017) kwa ajili ya kumuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa kuzindua Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP).

Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius Mheshimiwa Vishnu Lutchmeenaraidoo. Uzinduzi wa jukwaa hilo unatarajiwa kufanyika kesho mjini Port Louis ambapo utawakutanisha viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wanazuoni, wafanyabiashara pamoja na watu kutoka kwenye asasi mbalimbali za kiraia barani Afrika.

Pamoja na kuhudhuria mkutano huo, pia Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Mauritius litakalofanyika Machi 23, 2017.

Aidha, Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza mkutano huo anatarajia kutembelea maeneo maalumu ya uwekezaji, viwanda vya sukari na nguo. Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Khalid Salum Mohammed na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa . Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine wa Serikali.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: