wanamziki wa bendi ya mjengoni wakiwa wanafanya mambo ndani ya jukwaa la kiwanja cha nyumbani mjengoni Klabu
Rais wa bendi ya mjengono Robert Mukongya (Digital) akiwa anaimba ndani ya jukwaa
Habari picha na Woinde Shizza, Arusha.
Bendi mpya ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mjengoni classic band inatarajia kufanya utambulisho wao rasmi kwa mara ya kwanza mapema march 16 katika ukumbi wa Triple A klabu house uliopo ndani ya jiji la Arusha.
Akiongea na waandishi wa habari Rais wa bendi hiyo Robert Mukongya (Digital) alisema kuwa pamoja kuwa bendi hiyo imekuwa ikitoa burudani katika uwanja wa nyumbani mjengoni Klabu pamoja na sehemu nyingine mbalimbali lakini walikuwa awajaizindua rasmi hivyo wanatarajia kufanya uzinduzi ramsi katika siku hiyo ya alyamisi.
Alisema anapend akuwakaribisha wapenzi wote wa muziki wa dance wazee kwa vijana kuja kuona jinsi bandi hii inavyofanya kazi na jinsi bandi hii inavyotoa burudani kwa mashabiki wake huku akisisitiza waje waone staili mbalimbali za mziki zinazochezwa na wanamuziki wa bandi ya mjengoni.
Kwa upande wake mkurugenzi wa bandi hiyo John Mdenye alisema kuwa bendi yake imeimarika na wanamziki wanajiamini na ndio maana wameamua kufanya uzinduzi kwa mara ya kwanza rasmi ili wakazi wa mkoa wa Arusha waweze kuaidi mziki wa dance wenye viwango.
Alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa jiji la Arusha wenyeji na wageni pamoja na wale wanaotoka katika mikoa ya jirani kuhuthuria onyesho hilo kwani bendi yake imejipanga kuwapa burudani ya nguvu ambayo itaacha historia kwani show ambayo wataifanya amna bendi ingine yeyote imeshawai kufanya kama hiyo.
Alisema kuwa bendi hiyo imejipanga kuanza kutoa burudani majira ya saa moja usiku adi majogoo ,yote hiyo ni kuakikisha wapenzi wa mziki wa dance wanacheza adi pale hamu yao itakapo isha
Toa Maoni Yako:
0 comments: