Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi Hospitali ya Mirembe, Prof. Gadi Kilonzo akiongea na Wajumbe wa Bodi ya Hospitali hiyo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma.
Mganga Mkuu na Katibu wa Bodi ya Hospitali ya Miremb, Erasmus Mndeme akiongea na Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Hospitali ya Mirembe, Bibi. Doroth Gwajima akiongea na Wajumbe wa Bodi leo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma.
---
SERIKALI imesema kwamba tatizo la maradhi yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya akili yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku huku vyanzo vyake vikiwa ni pamoja na urithi, matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, matatizo ya kisaikolojia pamoja na hali ngumu ya maisha.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akizindua Bodi ya Hospitali ya Mrembe Mkoani hapo.

Akiongea na mbele ya Watendaji wa Bodi hiyo, wageni waalikwa pamoja na Viongozi wa hospitalini hapo, Waziri Ummy amesema kuwa, kundi lililoathirika Zaidi na kdhai hiyo ni vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa, ambapo alitaja taarifa ya Shirikala Afya Ulimwenguni (WHO) ya mwaka 2016n inayoonyesha takribani watu milioni 15.3 Duniani wanapata matatizo ya kiafya yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi.

“Matatizo haya yamekuwa yakisababisha vifo milioni 3.3 kila mwaka Duniani kote, hata hivyo taarifa ya Wizata yangu inaonyesha kwamba idadi ya watu wanaougua magonjwa ya akili inaongezeka kwa kasi kubwa kutoka wagonjwa 136,710 mwaka 2011/2012 hado wagonjwa 448,997 mwaka 2015/2016”, alisema Ummy.

Ameongeza kuwa, takwimu za hospitali ya Mirembe zinaonyesha kuwa, katika kipindi cha miaka mine kuanzia mwaka 2012 hadi 2016, jumla ya wagonjwa Zaidi ya 60,000 wenye magonjwa ya akili na waathirika wa dawa za kulevya walipatiwa huduma za afya na utengamao.

Aidha, kwa kutambua majukumu makubwa ya hospitali hiyo na kutatua changamoto zinazohusiana na magonjwa hayo, Serikali imeamua kuunda Bodi ya hospitalini hapo lengo likiwa ni kutekeleza dhana ya Utawala Bora na Utoaji wa Huduma Bora za Afya ya Akili kwa mujibu wa mapango mkakati na sera za nchi.

“Ninayo furaja leo kushiriki nanyi katika uzinduzi wa Bodi hii ya Hospitali ya Afya ya Akili Mirembe, na bodi hii itaongozwa na Mwenyekiti pamoja na Wajumbe waliouteuliwa kutoka maeneo mbaimbali ya kiujuzi hapa nchini”, alisema Waziri Ummy.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: