Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, akionesha kifurushi kilichohifadhi dawa za kulevya aina ya heroine iliyokamatwa wakati wa oparesheni ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya iliyofanyika kuanzia Februari 18, mwaka huu sambamba na ukamataji wa viroba 39 vya bangi pamoja na mirungi kama alivyokuwa akiwaonesha waandishi wa habari Februari 20, mwaka huu kwenye uwanja wa Jengo la Polisi la mkoa huo.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, akitoa taarifa ya operesheni ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa waandishi wa habari , Februari 20, mwaka huu ofisini kwake .
Gari aina ya Totota Noah yenye namba za usajili T. 799 BUG ikiwa imeshikiliwa na Polisi baada ya kukmatwa ikisafirish bangi viroba 21 kutoka katika kijiji cha Lubungo, Kata na Tarafa ya Mikese, wilaya ya Morogoro kwenda Jijini Dar es Salaam.( Picha na John Nditi).
Na John Nditi, Morogoro.
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limewatia mbaroni watu 66 kwa tuhuma za makosa ya kupatikiana na dawa za kulevya aina za heroine, mirungi na bangi viroba 39.
Watuhumiwa hao walikamatwa wakati wa operesheni maalumu dhidi ya mapambano ya dawa za kulevya iliyofanyika kuanzia Februari 19, mwaka huu kutoka wilaya za mkoa wa Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema hayo Feb 20, mwaka huu ofisini mwake wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya operesheni inayoendelea kufanyika kuhusu mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwenye wilaya za mkoa huo.
Matei alisema , watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili
Toa Maoni Yako:
0 comments: