Baadhi ya washiriki katika mkutano wa maendeleo ya mkoa (RCC)wa Arusha kama wanavyonekana pichani.
Aliyeshika kipaza sauti ni mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli akiwa anachangia mada katika mkutano huo wa( RCC)mkoani Arusha.
Na.Vero Ignatus Arusha.
Jamii za wafugaji katika mkoa wa Arusha wameshauriwa kubadili mfumo wao wa maisha ili kutojikaribishia baa la njaa litakaloathiri ustawi wa jamii zao.
Hayo yameelezwa na washiriki mbalimbali ambao wamehudhuria kikao cha Ushauri wa Mkoa (RCC) ambacho kimewashirikisha wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Arusha pamoja na wakurugenzi.
Akichangia mada mkuu wa wilaya ya Longido bwana Daniel Chongolo amesema jamii ya wafugaji wamekariri katika wilaya wilaya hiyo, chakula kilichopo nimahindi ambapo wangeliweza kutojishughulisha kutafuta vyakula vingine kama viazi, mtama na ndizi ambazo vinapatikana kwa wingi kwenye minada hasa ile ya Nanja na Selela.
Pia ameshauri jamii za wafugaji kua na utaratibu wa kujiwekea akiba ya chakula hasa wakati ule bei ya mifugo iko juu kwani wanaweza kuuza sehemu ya mifugo yao na kununua chakula cha kutosha na kuhifadhi katika maghala ya umma yaliyopo wilayani humo.
Hoja hiyo imeonekana ikichangiwa na wakuu wa wilaya zingine ambapo mkuu wa wilaya ya Ngorongoro amesema katika utafiti aliofanya katika wilaya yake kwenye minada mbalimbali bei ya mahindi imepanda kutofautisha na vyakula kama ndizi na viazi, kwakua jamii hizi hazina mazoea ya kula vyakula basi hulalamika ya kwamba kuna baa la njaa.
Akichangia mjadala huo mkuu wa mkoa wa Arusha amewataka wadau hao wa mkoa kuwa huru kuchangia, kushauri na kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika mkoa wao.
Kikao hicho kitaendelea tena kesho katika ukumbi wa mikutano wa mkoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: