Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akikagua mfumo wa kielektroniki wa ukadiriaji na ulipaji kodi ya ardhi Wilayani Kilolo mkoani Iringa mara baada ya kuwasili wilayani humo mapema wiki hii kufuatilia utendaji wa sekta ya ardhi. Dkt. Mabula pia alikagua kumbukumbu za majalada za ulipaji kodi.Anayetoa maelezo ya ufanyaji kazi wa mfumo huo ni Afisa Ardhi wa Halmashairi ya Wilaya hiyo Bw. Elinaza Kiswaga.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akisalimiana na wajumbe wa Baraza la Kata ya Mtitu Wilayani Kilolo mkoani Iringa mara baada ya kuwasili wilayani humo kufuatilia utendaji wa sekta ya ardhi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Kata ya Mtitu Wilayani Kilolo mkoani Iringa Bibi Veronica Salangeni ambaye amemaliza muda wake.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akikagua mfumo wa kielektroniki wa ukadiriaji na ulipaji kodi ya ardhi katika Wilaya ya Iringa Mjini mkoani Iringa alipotembelea kufuatilia utendaji wa sekta ya ardhi. Anayetoa maelezo ya ufanyaji kazi wa mfumo huo ni Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Shadrack Haule. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Bw. Richard Kasesela.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: