Wachezaji nyota wavulana wa Airtel Rising Stars wakiwa na Mkurugenzi wa
ufundi wa soka la vijana TFF na kocha wa zamani wa timu ya taifa , Kim
Paulsen mara baada ya kuwasilia kambini kwaajili ya mafunzo ya muda wa
wiki moja.
Wachezaji bora walioibuka kutoka katika mashindano ya Airtel Rising Stars msimu wa sita wamewasili rasmi leo kambini ili kuhudhuria mafunzo ya soka yaliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).
Mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa wiki moja yanayotegemea kuanza kesho chini ya makocha wa timu za taifa za vijana yatashirikisha wachezaji nyota 65 kutoka katika mikoa mbalimbali iliyoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars mwaka jana.
Akiongea na waandishi wa habari wakati kikosi hicho kilipowasili , Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF , Salim Madadi alisema” Tumejipanga vyema kupokea wachezaji hawa na kuwanoa ili kuendelea kutafuta vipaji kwa ajili ya timu zetu za vijana za taifa, ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya ya muda mfupi yatawasaidia vijana hawa kupata mbinu za mpira lakini pia kuziwezesha timu zetu kupata wachezaji bora kwaajili ya vikosi vyao.”
Mmoja kati ya wachezaji walioingia kambini hapo Amrani Rajabu Kutoka Mogogoro Alisema” ninafurahi kuona kambi hii inafanyika kama tulivyoahidiwa na kwakweli najisikia furaha kuwa mmoja kati ya wachezaji waliofanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars mwaka jana. Nimejipanga kutumia fursa vyema kwani naamini huu ndio mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa mchezaji nyota duniani. nawashukuru sana Airtel kwa kuanzia mpango huu na kutupatia nafasi ya kuonyesha vipaji vyetu.”
Wachezaji waliowasili kambini ni pamoja na Anthony Alfred (Mbeya), Amrani Rajabu (Morogoro), Yassin Ally (Temeke), Adam Almasi (Temeke), Mustafa Mhando (Kinondoni), Nickson Dimoso (Morogoro), Salum Mgonza (Kinondoni), Abdul Hassan (Morogoro), Benjamin Kawambwa (Mbeya), Yusuf Abdul (Temeke), Ibrahim Ngoitame (Morogoro), Mathias Juan (Ilala), Kambi Ramadhan (Kinondoni), Daniel Ndalo (Mwanza), Salum Yohana (Kinondoni), Esmail Kovu (Temeke), Munir Mzee (Ilala), Idrissa Omar (Ilala), Patrick Reuben (Morogoro), Ramadhan Gido (Mwanza), Said Maulid (Temeke), Ally Hamisi (Kinondoni), Nyamawi Athumani (Morogoro), Jabir Masumbuko (Morogoro), Tepsi Evance (Morogoro), Ernes Kamage (Mbeya), Gustafa Simon (Ilala), Ramadhan Chundo (Temeke), Hassan Kapera (Kinondoni), Juma Abdul (Ilala), Lameck Juma (Mbeya), Shabani Mangula (Kinondoni), Michael Joseph (Mwanza), Boniface Makala (Morogoro), Abdillah Kihulo (Temeke), Albinius Haule (Mbeya) kwa wanavulana na wasichana ni pamoja na Agatha Joel (Temeke), Fadhila Esmail (Arusha), Zubeda Mohammed (Kinondoni), Faraja Hamadi (ilala), Eva Jackson (Temeke), Violet Thadeo (Temeke), Zainabu Mrisho (Kinondoni), Fumu Mohammed (Ilala), Asphat Kasindo (Temeke), Elizabeth Julius (Temeke), Stella Wilbert (Kinondoni), Hawa Ally (Zanzibar), Christina Samuel (Temeke), Anna Anrea (Kinondoni), Grace Yusuf (Ilala), Shamimu Hamisi (Temeke), Mwantumu Ramadhani (Kinondoni), Hadlfa Mussa (Lindi), Zainabu Mrisho (Ilala), Fatuma Yusuf (Ilala), Eva Michael (Arusha), Oppa Msolidi (Temeke), Yustina Mboje (Temeke) na Zainabu Mohammed (Ilala).
Toa Maoni Yako:
0 comments: