Meneja mauzo Airtel mkoa wa Dodoma, Hendrick Bruno (kushoto) akiongea na Fikiri Chinji (kulia) anayejishughulisha na ufundi seremala juu ya maendeleo na changamoto za biashara baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha”, wakati Airtel ilipotembelea kwenye karakana yake katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa ya Dodoma ili kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi ya kuboresha zaidi biashara yake.
Meneja mauzo Airtel mkoa wa Dodoma, Hendrick Bruno (kulia) akishuhudia matumizi ya moja ya vifaa alivyowezeshwa kijana Fikiri Chinji anayejishughulisha na ufundi seremala kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” miezi tisa iliyopita, wakati Airtel ilipotembelea kwenye karakana yake katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa ya Dodoma ili kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi ya kuboresha zaidi biashara yake.
---
Kampuni na Taasisi mbalimbali hapa nchini zimeaswa kuiga mfano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kuwawezesha vijana mbalimbali kujiajiri wenyewe kupitia mradi wa Airtel Fursa,ili kupunguza tatizo la Ajira hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na mmoja kati ya waliofaidika na mradi wa Airtel Fursa kijana mjasiriamali anayejihusisha na fani ya ufundi seremala Fikiri Chinji aishie katika kijiji cha Ng”ong”ona manispaa ya Dodoma wakati alipotembelewa na Airtel ili kutadhimini maendeleo yake.

Fikiri alisema wapo vijana wengi ambao wapo mtaani wakitafuta ajira na wengine wakikumbwa na changamoto za mitaji ili kuendesha biashara zao, program kama hii ya Airtel Fursa ni vyema ikafanywa na makampuni mengi ili kuinua uchumi wa vijana jamii nan chi kwa ujumla

Mpaka sasa nawashukuru sana Airtel kwa kuniwezesha mtaji ambao umeweza kuinua biashara yangu, kupitia program hii nimeweza kutanua biashara yangu ya ufundi selemala na kuanzisha biashara ya welding. Sambamba na kutanua biashara pia nimeweza kuajiri vijana saba na kuongeza vifaa vingine zaidi, nawashukuru Airtel kwa kunishika mkono.”

Akizungumza katika eneo hilo Afisa Airtel kanda ya kati, Hendrick Werner amesema kijana Fikiri Chinji ameweza kupiga hatua kwa kuongeza vifaa vingine toka alipowezeshwa na Airtel Fursa, kukuza biashara pamoja na kutengeneza ajira kwa vijana wengine na kuwataka vijana wengine kuiga mfano wa fikiri kwa kuanzisha vikundi mbalimbali na kuwatafuta wadau watakao wawezesha kupita program mbalimbali ikiwemo hii ya Airtel Fursa.

Airtel Fursa ni mradi wa kijamii wenye dhumuni la kuhamasisha vijana, kuwapa nafasi ya kujiendeleza kibiashara na ujuzi utakoawawezesha kuimarisha biashara zao. Pambana group ni kikundi kingine kilichonufaika na mradi wa Airtel Fursa Dodoma ambacho kina vijana zaidi ya 15.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: