Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo
akizungumza na Blogu ya Jamii ya Michuzi juu ya uhakiki wa Tin Namba
leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Mapato
Nchini (TRA) imesema uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi ‘TIN
Number’ kwa Mkoa wa Dar es Salaam na umekwisha na uhakiki mwingine
utahamia Mikoa mingine.
Akizungumza na Blogu ya Jamii
ya Michuzi ,jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema uhakiki TIN Number muda wake
ulikuwa ikiongezeka kutokana na mahitaji.
Kayombo
amesema kuwa kwa sasa muda hautaongezwa na wenye Tin number
hawatakiwi kutumia mpaka pele watapopata maelezo katika ofisi za TRA
ili waweze kuendelea kutumia namba hizo.
Sehemu baadhi ya wananchi wakiwa katika uhakiki wa TIN namba leo jijini
Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii).
Amesema uhakiki huo ulianza Agasti hadi Oktoba na kuongeza tena muda wa miezi mitatu ambao umeishia leo.
Kayombo amesema kuwa wale ambao wana Tin number na zinadaiwa TRA wanazo na wanatakiwa kulipa kodi zao ambazo wanadaiwa.
Amesema uhakiki wa Number wa unasaidia kupata taarifa za mfanyabiashara kwa kwa namba ya simu, makazi, sehemu anayofanyia kazi pamoja na anuani za mlipa kodi.
‘’Watu wote wenye Tin Number wasizitumie mpaka pele watapokuwa wamepata maelezo juu ya kuzitumia namba hizo za utambulisho wa wafanyabiashara’’ amesema Kayombo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: