Afisa Habari wa kampuni ya mabasi yaendayo Haraka (UDART), Deus Buganywa akizungumza na waandishi habari juu ya uzinduzi mradi wa mabasi yaendayo haraka kesho jijini Dar es Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jami.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Rais Dk. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (UDART) katika kituo cha mabasi Gerezani –Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa kampuni ya mabasi yaendayo Haraka (UDART), Deus Buganywa amesema katika uzinduzi barabara ya Msimbazi itafungwa na mabasi yatakwenda kugeuzia katika kituo cha Feri.

Amesema safari za mabasi zitasitishwa mpaka pale uzinduzi utakapo kuwa umekwisha na kurejea katika hali ya kawaida.

Buganywa amesema kwa abiria wanatumia kituo cha Gerezani watashuka katika kituo cha zimamoto ‘Fire’ na mabasi hayo yataendelea mpaka kituo cha Feri.

Kampuni ya mabasi hayo inawaomba radhi abaria wanaoshuka katika vituo vya msimbazi hadi Gerezani kwa usumbufu ulioitokeza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: