Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya maji takaDar es Salaam (DAWASCO) Mkoa wa Ilala imeanzisha mpango kabambe wa kupambana wa kupambana na Kero na changamoto za utoaji huduma kwa kufungua DAWATI LA DAWASCO kwenye serikali za Mitaa.

Akizungumza na Globu hii Meneja Dawasco mkoa wa Ilala Christian Kaoneka amesema kuwa dawati hilo litasaidia kulinda mfumo na kupunguza kero kwa wananchi kwa kudhibiti mivujo, kwa kushirikiana na viongozi wa mitaa na Madiwani ambao wengi wao wapo karibu na wananchi.

Akizungumza na Globu ya Jamii Mtendaji wa kata ya Kivukoni alimshukuru Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja kwa kuwaletea Uongozi Mpya katika Mkoa wa Ilala ambao umekuwa ukifanya kazi kwa karibu kabisa na serikali za Mitaa, hii inapelekea kushiriki moja kwa moja kuzifikia kero na kupeleka huduma kwa Wananchi,

"Uongozi wa Sasa umekuwa karibu kabisa na sisi viongozi na wananchi katika kutatua kero za wananchi moja kwa moja, changamoto bado zipo nyingi ila taratibu tumeanza kuona matunda yake, naamini kabisa uongozi ukiendelea hivi kwa asilimia kubwa tutapunguza malalamiko kwa wananchi"

Naye mmoja wa wananchi katika Kata ya Gerezani aliushukuru uongozi wa DAWASCO Mkoa wa Ilala kwa kuanza utatuzi wa kero ya muda mrefu ya Maji Taka katika eneo la Collesium

"Kero hii ilikuwa ni ya muda mrefu sana, lakini nimeona sasa hatua zimeanza kuchukuliwa, Dawasco wamefika na ukarabati wa ile Line ambayo ilikuwa inasababisha Maji Taka kumwagika hovyo barabarani imeanza kukarabatiwa, Tunaishukuru sana DAWASCO"

Naye Meneja wa DAWASCO Mkoa wa Ilala Ndugu Christian Kaoneka amesema wanazidi kwenda kuwafikia wananchi ambao ndiyo walengwa wakubwa wa Huduma kwa kuanzisha Dawati la DAWASCO katika serikali za Mitaa

Amesema ufunguzi wa dawati hili unafungua fursa ya kila mwananchi kuwa huru kueleza utendaji wa Dawasco Ilala aidha kutakuwa na mtu maalum wa kupokea maunganisho mapya kwa wateja wapya na changamoto zote kama vile mivujo, taarifa za uharibu wa miundo mbini yetu na taarifa za wizi wa Maji.

Amesema kuwa changamoto bado zipo nyingi hivyo anawaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha hasa katika swala zima la usafi wa mazingira katika mifumo ya Maji Taka kwa kuwaomba wasitupe mifuko ya Plastiki hovyo pia waweze kusaidia kufichua watu wote wanaojiusisha na wizi wa maji.

Pia Ndugu Kaoneka amesema DAWASCO Ilala inakwenda kufanya Uhakiki Upya wa Wateja wake wanaotumia huduma yao ya Maji Safi na Maji Taka, hivyo basi ameomba ushirikiano kwa wananchi wakati wa zoezi hili

"Tunaenda Kuhakiki upya wateja wetu wa Maji safi na Maji Taka, tunajuwa kabisa zamani Maji yalikuwa machache na wengi wa wananchi katikati ya Mji hawakupata huduma yetu kwa kipindi kirefu hali iliyopelekea kuchimba visima, ila kwasasa uzalishaji umekuwa mkubwa sana kwani Mitambo yetu yote ya Ruvu Juu na Ruvu Chini inafanya kazi vizuri, hii imepelekea ongezeko la Maji, kwahiyo tunaamini kwamba maji yetu yanafika katikati ya mji kwa asilimia kubwa, hivyo wewe Mtumiaji wa Huduma yetu ambaye unasingizia una huduma ya kisima wakati unatumia maji yetu ukikutwa tutakuchukulia kama Mwizi wa Maji ambalo ni kosa Kisheria, na kama kweli unatumia kisima tutaomba uache documents zote zenye kuonyesha uhalali wa kisima chako, maana wote tunatambua visima vyote vina usajili chini ya wakala wa visima" alisema Bwana Kaoneka

Ametaja kuwa atayari ameshakutana na baadhi ya viongozi wa Kata kama vile Upanga Mashariki na Upanga Magharibi, Buguruni na Gerezani, kwa ajili ya kuimarisha operesheni hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: