Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairuki akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happi wakati wakikagua mradi wa TASAF.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairuki akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happi katika moja ya kaya masikini inayosaidiwa na mradi wa TASAF.
---
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairuki leo amefanya ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAF.

Mh. Kairuki alianza ziara hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa hua Mh. Ally Hapi.

Akiwa ofisini hapo Mh. Kairuki alisaini kitabu cha wageni na kusalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Ally Hapi, wakuu wa wilaya za Ilala, Temeke, Kigamboni na Katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam.

Mara baada ya kusaini kitabu cha wageni, Mh. Angela Kairuki alifanya mkutano na wakuu wa wilaya, wakurugenzi na waratibu wa TASAF Mkoa na manispaa za Dar es salaam ambapo alipokea taarifa mbalimbali za manispaa na Mkoa mradi wa kuondoa umasikini wa TASAF.

Katiba hotuba yake Mh. Kairuki amewataka waratibu wa TASAF wa Mkoa na manispaa kujipanga vema, kusimamia mradi kwa makini na kuondoa wale wote wasiostahili kupata fedha hizo katika orodha ya wanufaika wa TASAF.

Akitoa salam za Mkoa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Ally Hapi amemshukuru Mh. Kairuki kwa ziara hiyo na kumfahamisha kuwa Mkoa wa Dar es salaam unakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa TASAF ikiwemo watu wasiostahili majina yao kuingizwa miongoni mwa wanufaika, kuingizwa kwa majina hewa, kubaguliwa kwa baadhi ya wananchi masikini kwa itikadi za kisiasa na ufuatiliaji duni unaofanywa na waratibu wa TASAF ngazi mbalimbali.

Ziara ya Mh. Angela Kairuki iligusa pia maeneo ya Kata za Kigogo na Msasani ambako Mh. Waziri alipata nafasi ya kuongea na wananchi wanufaika wa TASAF katika mikutano ya hadhara mitaa ya Kigogo Kati na Mikoroshini (Msasani).

Wananchi waliojitokeza wameishukuru serikali kwa mradi huo ambao umekua msaada mkubwa kwao katika kujikwamua na umasikini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: