Baadhi ya washiriki wa Shindano la Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili Hoteli ya Regency Msasani jijini Dar es Salaam leo kuanza kambi rasmi.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com).
Mkurugenzi wa Lino Agency, waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundega akizungumza na waandishi wa habari hotelini hapo mara baada ya idadi kubwa ya warembo hao kuwasili tayari kuanza kambi rasmi. Kushoto ni Mkuu wa Itifaki Albert Makoye na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Miss Tanzania, Deo Captain.
Warembo wakiwasili kwenye Duka na Mgahawa wa Kampuni ya Tomoni Farm, la 'The Farm Fresh Market', maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaam kujionea shughuli mbalimbali zifanywazo na kampuni hiyo, pia kujipatia chakula cha mchana.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla, akiwapatia maelezo warembo hao walipotembelea duka la kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya warembo wa Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla (katikati), nje ya duka la The Farm Fresh Market, Victoria jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla (katikati), akiwapatia maelezo warembo hao, wakati akiwambeza kwenye sehemu mbalimbali za kampuni hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya warembo wa Miss Tanzania wakiangalia Menu walipofika Mgahawa wa Kampuni ya Tomoni Farms, Victoria jijini Dar es Salaam leo.
JUMLA ya washiriki 30 wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania wameanza kambi ya mwezi mmoja leo tarehe 30 Septemba 2016 jijini Dar es Salaam.
Washiriki hao ambao ni washindi kutoka Kanda 9 na mikoa mbalimbali Tanzania watapokelewa katika Hotel ya Regency Park iliyopo Mikocheni D’salaam, na baadae watapiga kambi ya siku 4 katika Hotel ya Jozi Lounge iliyopo Msasani jijini D’salaam.
Mara baada ya kuingia kambini washiriki hao 30 pamoja na Wasimamizi wao watakuwa na Semina ya pamoja ambapo watafundishwa masuala mbalimbali yahusuyo mashindano pamoja na kambi kwa ujumla.
Wakiwa kambini washiriki hao watafanya ziara katika mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha, Geita na Mwanza kwa shughuli mbalimbali za kijamii.
Kauli mbiu ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 ni Urembo na Mazingira Safi, hivyo washiriki wote watafanya kazi mbalimbali kijamii ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira, kutunza mazingira na pia kushiriki katika kampeni ya kupanda miti itakayofanyika tarehe 1 Oktoba 2016 nchini pote.
Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 yamekuwa na changamoto kubwa ya kupata wadhamini wachache waliojitokeza kudhamini mashindano haya katika mikoa na sehemu mbalimbali.
Tunachukua fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Wadhamini wote waliojitokeza na kuchangia kwa njia mbalimbali katika kufanikisha mashindano ya mwaka huu.
Tunawashukuru pia washiriki wote katika ngazi zote waliojitokeza kushiriki na pia shukrani kwa wazazi na walezi walioruhusu watoto wao kushiriki mashindano ya urembo ya miss Tanzania 2016.
Ni matarajio yetu kwamba wadau wote wa tasnia hii ya urembo nchini mtajitokeza kwa wingi katika Fainali za Shindano la Miss Tanzania 2016 linalo tarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2016.
Toa Maoni Yako:
0 comments: