Mkurugenzibwa TAMWA, Edda Sanga akizungumza na wanahabari wakati wa ufunguzi wa semina elekezi ya namna ya kuandika habari za Usalama Barabarani kwa uweledi iliyoanza okotba 18-20.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) usalama barabarani Mary Kessy akielezea jambo wakati wa semina elekezi kwa waandishi wa habari namna ya kuandika taarifa za usalama barabarani kwa uweledi
 Mwanzilishi wa Chama cha Wanahabari wanawake (TAMWA) na mtangazaji wa Shirika la Idhaa ya Kiswahili ya Uingereza (BBC) Valeria Msoka akizungumza na wanahabari wakati wa semina hiyo na namna ya kukabili ajali za barabarani na nini kifanyike ili kutokomeza.
---
Na Zainab Nyamka , Globu ya Jamii.

CHAMA cha Wanahabari Wanawake Nchini (TAMWA) kimeendelea kuwapiga msasa waandishi wa habari kuhusiana na namna ya kuandika na kuripoti taarifa za usalama barabarani.

Akifungua semina hiyo jana, Mkurugenzi wa TAMWA Edda Sanga amesema kuwa mradi wa usalama barabarani unaendeshwa hapa nchini kupitia TAMWA na taasisi nyingine lengo kubwa ni kuona kwamba wanahabaribwanapata weledi wa kuandika habari hizi kwa mapana yake hasa wakizingatia wanatoa elimu kwa jami.

Sanga amesema, kutokana na idadi kubwa inayosababishwa na ajali za barabarani, TAMWA imeona ni muhimu kulibalia njuga na kushirikiana na wadau wengine ikiwemo wanasheria kuweza kuhakikisha sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973 inafanyiwa marekebisho kwani itaweza kudhibiti watumiaji wanaokiuka matumizi sahihi ya barabara.

Maeneo yanayohitajika kufanyiwa marekebisho ni mwendokasi kwa magari ya abiria na binafsi, ulevi wakatinwa uendeshaji, uvaaji kofia ngumu (helmet) kwa madereva wa bodaboda na kufunga mikanda na vizuizi kwa watoto ambapo sheria hizo hazimbani mtumiaji wa chombo cha moto katika sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973.

Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia mradibwa Blomberg Initiative for Globa Road Safety (BIGRS) Mary Kessy amesema kuwa Tanzania ni moja ya nchi tano iliyonufaika kwa mradi huo ambao umelenga katika kuhakikisha wanatokomeza ajalibza barabarani kwa kipindi cha miaka mitano hasa ukizingatia takribani watu 3400 wanafariki wa siku kutokana na ajali za barabarani sawa na milioni 1.25 kwa mwaka.

Takwimu inaonesha kuwa katika alimia 49 za visababishi vya ajali asilimia 23 ni pikipiki, asilimia 22 ni za watembea kwa miguu huku aslimia nne ni waendesha baiskeli na katika ajali hizo umri unaoathirika zaidi ni kati ya miaka 15-29 na kwenye kila ajali nne wanaume wanakuwa ni watatu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: