Hawa ndio baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya Malangali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika shule hiyo na kukaangalia mazingira ya shule hiyo na kutafuta njia za kutatua baadhi ya changamoto kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania
Mkurugenzi wa kampuni ya Yono Action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) akizungumza mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Malangali na kuwaeleza jinsi gani shule hiyo ilivyowapa mafanikio hadi sasa walipofikia.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Malangali iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamewataka vingozi, wafanyabiashara, wakulima na wajasiliamali mbalimbali walinufaika na elimu kutoka shule ya malangali kurudisha fadhila katika shule hiyo.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kampuni ya Yono Action Mart Yono, Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) alisema kuwa maendeleo aliyoyapata sasa ni kutoka na shule ya mangali hivyo ameamua kurudi na kuisadia shule hiyo.
“Wafanyakazi na viongozi mbalimbali tunatakiwa kuboresha mazingira na miundombinu ya shule tulizosoma ili kuendeleza na kukuza elimu ya hapa nchini tanzania.” Alisema Kevela
Kevela amesema kuwa shule nyingi walizosoma viongozi,wafanyabiasha na wajasiliamali mbalimbli zinahitajika kukarabatiwa hivyo amewataka wadau wote kuzikumbuka shule walizosoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments: