Mkufunzi na mjumbe wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini Henry Tandau akielezea jambo mbele ya wanahabari waliohudhuria semina elekezi ya masuala ya Usalama Barabarani na jinsi ya kuandika matukio hayo.
Mkurugenzibwa TAMWA, Edda Sanga akizungumza na wanahabari amesema kuwa hali bado si nzuri katika suala zima la usalama barabarani.
Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) usalama barabarani Mary Kessy akielezea jambo.
Waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo hayo.
---
Takriban asilimia 85 ya nchini zote duniani zimegundulika kuwa hazina sheria madhubuti za kuondokana na ongezeko la vifo vinavyotokana na ajali za barabarani.
Takwimu hizo ni Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na shirika la afya Duniani WHO mwaka 2015 ambapo imebainika kuwa takriban vifo million 1.25 hutokea kila mwaka dunia kutokana na ajali za barabarani ambapo Afrika inaongoza kwa asilimia kubwa.
Akizungumza katika semina ya usalama barabarani ambayo iliandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) Mkurugenzi wa chama hicho Mama Edda Sanga amesema kuwa hali bado si nzuri katika suala zima la usalama barabarani.
“Kwasasa kuna ajila nyingi zimepitiliza duniani ambapo zaidi ya majeruhi million 20 hutokea kila mwaka kwa ajali za barabarani ambapo nchi za afrika zinaongoza kwa asilimia 90 na hiyo inatokana na na kutokuwa na sheria ya usalama barabarani iliyomadhubuti”
Kwa upande wake Mary Richard ambaye ni wakili Toka Chama cha sheria wanawake Tanzania TAWLA alisema kuwa sheria iliyopo ya usalama barabarani ya mwaka 1973 bado haihamasishi kufanya vizuri katika eneo hilo kwani haijaweka mkazo katika mambo mbalimbali.
“Sheria yetu ya usalama barabarini imekuwa na mapungufu mengi ambayo inampelekea mtekelezaji kushindwa kuitekeleza kama suala zima la uvaaji wa kofia ngumu(HELMET)kwa waendesha bodaboda haimemtaka mwendesha bodaboda pekee kuvaa kofia lakini si abiria jambo ambalo ni hatari kwa jamii”
Hata hivyo wananchi nao wameweza kutoa Maoni yao kuhusiana na sheria hiyo ya Usalama barabarani ya Mwaka 1973 ambapo wameunga mkono ubadilishwaji wake na kutaka kuangalia namna ya Kuiweka ili ajali za barabarani ziishe ifika 2020, John Mark alisema kuwa sheria bado haipo wazi hasa suala zima la utumiaji simu wakati wakuvuka barabara na kuendesha gari hivyo bila kuziangalia kwa mapana zaidi haiwezi kulinda usalama wa wananchi”
Je nini jitihada za wadau wa kisheria katika suala zima la sheria hii ya usalama wa barabara katika kuihamasisha serikali kuboresha sheria hiyo,wakili wa huduma za msaada wa kisheria TAWLA , Mary.anaeleza
“Alisema kuwa eneo lao kubwa wao ni kushawishi na kutoa elimu kutokana na utaratibu wa kubadilisha sheria ni serikali na Bunge”
Toa Maoni Yako:
0 comments: