Multichoice Tanzania imeamua kunufaisha wateja wake kwa kufanya mapinduzi makubwa kupitia punguzo la bei na kuongeza chaneli 8 kupitia huduma yake ya DStv. Huduma hizo mpya za punguzo la bei zitaanza rasmi kufanya kazi kuanzia tarehe 1 Novemba, 2016. Vifurushi hivyo vya DStv ni DStv Premium, Compact Plus, Compact, Family na Access. Punguzo hizo za bei ni kama ifuatavyo:
DStv Premium inapokea punguzo la asili mia 16%, kuanzia Novemba 1, na bei itakuwa TZS 184 000. Pamoja na hayo, ongezeko la chaneli 8. DStv Compact Plus, inapokea punguzo la asili mia 17%, na bei yake itakuwa TZS 122,500. Wateja wataendelea kufaidi burudani ya hali ya juu ya vichekesho, tamthilia, sinema, michezo na vinginevyo.
Chaneli hizo mpya zitakazorushwa ni Vuzu AMP, Lifetime, Discovery channel, Crime & Investigation, History channel and Africa Magic Showcase. DStv Compact Plus, imeongezewa chaneli za michezo zitakazoendeleza msisimko kwa wapenzi wa mpira wa miguu kupitia vipindi vya UEFA Champions Leagues, European Football leagues na Europa league. Hizo mechi zote zinapatikana kwenye stesheni za SuperSport 6 (SS6) na SuperSport 4 (SS4).
Kwa wapenzi wa filamu za kiafrika, watafaidi kupitia Nollywood , wapenzi wa tamthilia zakilatino wataburudishwa na telenovelas pamoja na filamu za Bollywood. Bila kusahau sinema zitakazopatikana kupitia chaneli za ROK, Eva Plus na B4U Movies.
DStv Compact inapokea punguzo la asili mia 5%, na bei yake mpya ni TZS 82 250. Kifurushi hiki kina faida ya kurusha Premier League na La Liga tangia mwanzoni mwa mwaka huu. Pamoja na hayo, wateja wa DStv wataongezewa chaneli za ITV Choice (DStv chaneli 123), TCM (DStv chaneli 137) na SS4. Kuanzia Novemba na kuendelea, wateja wa Compact watafaidishwa na chaneli za ROK, Eva Plus na B4U Movies!
Kifurushi cha DStv Family kimepokea punguzo la asili mia 16% na bei yake mpya ni TZS 42 900. Kifurushi hichi kinapokea ongezeko la chaneli 5, ambazo ni B4U Movies, Eva, Eva Plus, SS4 na FOX. Kifurushi cha DStv Bomba kitafaidisha wateja wake kwa ongezeko la chaneli 3, na punguzo la asili mia 15%, bei yake mpya ni TZS 19,950. Punguzo hili la bei kwa kifurushi hiki itaanzia tarehe 15 Novemba.
Katika mkutano huo, Mkurugenzi Ronald Baraka Shelukindo alisema yafuatayo: Nia yetu kuu katika kufanikisha punguzo hilo la bei ni kuweza kunufaisha wateja wetu ili kuwapa huduma bora zaidi na kuthamini mchango wao katika muendelezo wa kampuni yetu. Multichoice tunayo furaha kubwa pia kuwaalika wateja wapya ili waweze kufaidi kupitia huduma zetu. Mapinduzi haya ya punguzo za bei ni mwamko mkubwa sana katika kufanikisha malengo yetu sio tu hapa nchini, lakini Afrika nzima.
Toa Maoni Yako:
0 comments: