Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Juma Porini Keya (katikati) akitoa risiti ya malipo kwa kutumia kifaa cha kieletroni (POS).
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Juma Porini Keya (kushoto) akipokea maelezo toka kwa mkusanyaji wa mapato Charles Ghati katika mnada wa kijiji cha Rung'abure, Katikati ni Kaimu Mtunza Fedha Bw. Terry Hurson.
Wafanya Biashara wakifanya malipo katika mnada wa kijiji cha Rung'abure Kata ya Rungaabure Wilayani Serengeti.
---
“Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imefanikiwa kuongeza mapato yatokanayo na minada mbali mbali inayofanyika ndani ya Wilaya”

Hayo yamesemwa na Terry Hurson ambae ni Kaimu Mtunza Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti alipokuwa anazungumza na Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango waliofanya ziara katika Mnada wa Kijiji cha Rung’abure kilichopo Kata ya Rung’abure.

Ziara hiyo ya ukaguzi ni mwendelezo wa taratibu zilizowekwa na Serikali kwa kuwahusisha Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kutembelea miradi kila baada ya miezi mitatu (Robo Mwaka wa Serikali).

Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Porini Keya pamoja na Katibu wa Kamati hiyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Juma Hamsini pamoja na wajumbe wa Kamati walijionea jinsi ukusanyaji wa mapato unavyofanyika kwa kutumia vifaa vya kieletroniki (POS) vinavyotumika pia kutoa risiti za malipo. “Mapato ya Minada yameongezeka kutokana na kuzuia mianya ya ukwepaji wa kodi na matumiz ya POS” alisema Terry Hurson.

Ukusanyaji wa mapato unafanywa na watumishi wa Serikali, hii ni baada ya Serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuzitaka Halmashauri zote nchini kukusanya mapato na kuacha kutumia wazabuni katika kukusanya mapato kwenye masoko na minada.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: