Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imezindua wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kutambua umuhimu wa wateja wao na kuwapongeza watoa huduma wanaowahudumia wateja vizuri na kutatua mahitaji yao ya huduma za mawasiliano ya kila siku.
Mwaka huu wiki ya huduma kwa wateja itaanza leo jumatatu huku Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel Bi, Adriana Lyamba akisema “wiki ya huduma kwa wateja ni wiki muhimu sana kwa Airtel na ndio maana tumekuwa tukiiadhimisha kila mara kwa kuweka aina tofauti za matuko yanayolenga kutuweka karibu sana na wateja kwa kuwahudumia vyema. Mwaka huu tunatarajia kuendesha matukio tofauti wiki nzima kuanzia tarehe 3 -7 Octoba 2016 ikiwa ni namna ya kuwashukuru wateja kwa kuendelea kutumia huduma zetu na kuwakaribisha wateja wengine wanaohamia kwenye Familia ya Airtel
“Airtel tunathamini sana wateja wetu kwa kuwa wao ndio mhimili mkuu wa biashara yetu, na hii ndio sababu kubwa inayotufanya tutenge muda wote wa wiki hii kwa lengo la kupata maoni toka kwa wateja wetu juu ya huduma tunazotoa kwa lengo la kuendelea kuboresha bidhaa na huduma zetu ziendane na mahitaji ya wateja wetu yanayokua kwa kasi kila siku” alisema Bi Lyamba
“Kaulimbiu ya Mwaka huu ni ‘Service Champions’ yaani ‘Bingwa wa Huduma’ tutaitimiza kwa kuhakikisha tunatoa suluhisho kwa mahitaji ya wateja wetu sambamba na kutoa huduma za viwango vya juu zenye kuleta tija kwa jamii” Bi Lyamba alibainisha
Bi Lyamba aliendelea kusema.” Katika kusherehekea wiki hii na wateja wetu, Airtel tunajivunia kutoa huduma na bidhaa za kipekee na kibunifu, kupitia kampeni yetu ya “Sibanduki” tumewawezesha wateja zaidi ya million 10 kufaidika na huduma zetu na kuwapa sababu za kuendelea kutumia na kujiunga na huduma zetu. Huduma zetu za kipekee ikiwemo Vifurushi vya Yatosha, mikopo ya Timiza kwa wateja na Mawakala, kutuma pesa bure kwa kupitia Airtel Money, kufanya mihamala ya fedha yaani benki kwenda kwenye simu au kutoka kwenye simu kwenda banki yanaonyesha jinsi tulivyojikita katika kuhakikisha mteja anapata huduma za hali ya juu zinazokidhi mahitaji yake ya huduma za mawasiliano. Wateja wapya watakaojiunga na huduma zetu wiki hii kujiunga watapata dakika 160 za kupiga mitandao yote, sms 2000 na MB 200 Bure, kwa miezi miwili”
“tunawakaribisha wateja kutembelea maduka yetu ya Airtel au smarphone Bazaar pale Mlimani City ili kuweza kujipatia simu za kisasa za Smartphone kwa gharama nafuu sana
Airtel tumejipanga kuwahudumia kwa umakini ili kuweka kumbukumbu ya kwamba Airtel ni Bungwa wa kutoa huduma za Mawasiliano” alimaliza kwa kusema Bi Lyamba
Toa Maoni Yako:
0 comments: