Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MABINGWA watetezi
wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga wamelazimishwa suluhu ya bila magoli na
timu ya Ndanda mchezo uliochezwa Katika uwanja wa Nangwanda Sijaona
Mkoani Mtwara.
Mechi hiyo iliyoanza kwa kasi kila
upande wakitafuta goli la ushindi ilikuwa na kasi kubwa sana na
kupelekea faulo za mara kwa mara katika kipindi cha dakika 45 za mwanzo.
Dakika ya 25, Obrey Chirwa anakosa goli la wazi baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Donald Ngomana kuokolewa na mabeki.
Andrew
Vincent ‘Dante’ aliweza kuokoa mashambulizi mengi ya hatari ya Ndanda
pamoja na kuokoa mpira mmoja uliokuwa unaelekea nyavuni kufuatia shuti
la Omary Mponda.
Salum Minely anapewa kadi ya njano
baada ya kumfanyia madhambi Donald Ngoma huku Kigi makasy akizawadia
kadi pia baada ya kumchezwa rafu mbaya Saimon Msuva na kwa upande wa
Yanga Deus Kaseke anapatiwa kadi ya njano.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Yanga wakionekana kulisakama lango la Ndanda lakini umaridadi wa Safu ya Ulinzi unatibua mipangilio yao yote.
Yanga wanafanya mabadiliko ya kumtoa Deus Kaseke na kuingia Mahadhi ili kuimarisha safu ya kiungo huku dakika ya 66 Ndanda wanamtoa Salum Minely na kuingia Nasoro Kapama.
Dakika ya 90, Jeremiah Kisubi anadaka mpira na kuudunda chini na kisha kutembea nao ndani ya boksi na mwamuzi Hanse Mabena anaamrisha kupigwa pigo la ndani ya 18 na Yanga kupoteza nafasi iliyopelekea mpira huo kumalizika kwa suluhu ya bila magoli.
Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona sio rafiki kwani hauna ubora ndiyo maana wachezaji wake wameshindwa kucheza mpira ule uliozoeleka.
Amesema Mwambusi, kupata alama moja ugenini sio mbaya sana ila wanachokiangalia kwa sasa ni michezo inayofuata.
Yanga wanatarajiwa kuondoka kesho kurejea Dar es salaam kuvaana na Majimaji ya Songea mchezo utakaopigwa Jumamosi Uwanja wa Uhuru.
Toa Maoni Yako:
0 comments: