Maafisa watatu wa serikali na meneja ws CRDB tawi la Bukoba wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Bukoba wakituhumiwa kula nja kwa kufungua account ya bandia inayofanana na ile inayotumika kukusanya fedha za waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.
Aliyekuwa Ofisa tawala Mkoa wa Kagera (RAS) Bw Amantius Msole,Aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba BW Kelvin Makonda,AliyekuwaMhasibu wa Mkoa Kagera Simbaufoo Swai na Meneja CRDB Kagera Karlo Sendwa wamefikishwa mahakamani leo mchana kwa kutengeneza account bandia iliyo na jina sawa na lilioandaliwa na serikali kukusanya fedha kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko mkoani Kagera.
---
WATUMISHI watatu wa serekali akiwemo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Bukoba mjini wamepandishwa kizimbani jana na kusomewa mashtaka mawili  ya kutaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kufungua akaunti  feki ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye kesi namba 239/2016.

Watumishi  waliofikishwa mahakamani hapo leo ni aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa  Kagera Amantus Msole, mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Kelvin  Makonda, Muhasibu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai na Meneja wa banki ya CRDB Tawi la Bukoba Carlo Sendwa.

Akiwasomea mashtaka yao kwenye mahakama ya hakimu mkazi ya Bukoba  wakili wa serekali Hashimu Ngole alisema kuwa watuhumiwa hao  wanashitakiwa kwa makosa mawili kosa la kwanza ni watuhumiwa walikula  njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana  na jina la akaunti ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye no.015225617300 ,ambapo  wao walifungua akaunti yenye jina la KAMATI MAAFA KAGERA yenye namba  no.0150225617300 Alilitaja shitaka la pili kuwa ni watuhumiwa wanashitakiwa kwa kutumia madaraka na vyeo vyao vibaya kinyume cha sheria.

Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao walimwomba hakimu awapatie dhamana wateja wao kwakuwa bado ni watumishi wa serekali na wanao uwezo wa  kujidhamini wenyewe na hawawezi kutoka nje ya Kagera

Hakimu Mkazi wa mahakama ya Bukoba Denis Mbelemwa alihairisha kesho hiyo hadi kesho saa tatu asubuhi baada ya kupitia upya vifungu vya sheria na  kujiridhisha kama watuhumiwa wanasitahili dhamana na kutaka watuhumiwa  warudishwe rumande.

"Nahairisha shauri hili hadi kesho asubuhi  saa tatu nikapitie tena vifungu vya sheria, kutokana na ukubwa wa kesi  hii nione kama watuhumiwa wanadhaminika" alisema Hakimu Mbelemwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: