Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdul (kulia) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha wateja wa rejareja wa First National Bank (FNB), Francois Botha (kushoto) kwa niaba ya washindi kumi wa kampeni inayoendeshwa na benki hiyo kuhamasisha uwekaji akiba ili kujikwamua kiuchumi. Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es salaam leo.
Meneja Masoko wa First National Bank, Blandina Mwachang’a akiwapigia simu washindi wa droo ya kampeni inayoendeshwa na benki hiyo kuhamasisha uwekaji akiba ili kujikwamua kiuchumi ambapo washindi kumi walijipatia shilingi milioni moja kila mtu. Wengine kwenye picha ni Meneja wa Sheria wa benki hiyo, David Sarakikya (kushoto), Mtaalamu wa Mfumo wa Habari na Mawasiliano wa FNB, Bi. Ilakiza Hezwa na Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdul (kulia).
---
Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba iliyoendeshwa na First National Bank Tanzania imefika mwisho baada ya miezi mitatu ambapo. Kupitia droo ya mwisho ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam leo washindi kumi wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja.

Akiongea kwenye makabidhiano ya zawadi ya fedha hizo kwa washindi wa mwezi Agosti, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha alisema: “Kampeni ya Mama imekuwa na mvuto kwa watu wengi na wameweza kuitumia kujiwekea akiba benki. Sisi kama benki ni jukumu letu kuwatunuku wateja wetu kwa uaminifu wao kwetu na kuwapa nafasi ya kujiwekea akiba ya badae. Hii kampeni imekuwa na mafanikio makubwa na tumefurahia kuona wateja wetu wanajitokeza kwa wingi kushiriki.”

Kampeni ya Mama ilizinduliwa mwezi Juni ambapo katika muda wa miezi kampeni hiyo imetoa fursa ya kujishindia mamilioni ya fedha taslimu kutokana na kila shilingi elfu hamsini waliyokuwa wakijiwekea kwenye akaunti zao.

Botha alitaja washindi wa droo hiyo kuwa ni. Adolph Kalyelibwa wa Mwanza , Halima Mohamed wa industrial branch, Devotha Muttakywa wa Mwanza, Alvin Kamoyo wa Mwanza, Gilbert Mosha wa Mwanza, Denis Mazige wa Dar es salaam, Isiaka Said wa Mwanza, Gladys Cafrica wa Dar es salaam, Geradina Chipala wa Mwanza na Sumbuko Chipanda wa Dar es salaam.

Benki ya FNB ilianzisha kampeni ya Mama kwa lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiwekea akiba ambapo kupitia droo za kampeni hiyo kwa muda wa miezi mitatu jumla ya washindi 30 wamejishindia zawadi.

Botha alisema kwamba kampeni hii imejenga msingi mzuri kwa kuijengea jamii utamadani wa kuweka akiba kwa ajili ya badae na vilevile ni msingi mzuri wa kupata maisha bora kutokana na kuwa na akiba ya kuwekeza katika maendeleo na kuboresha maisha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: