Leo katika Ofisi za Wamarekani wa Kujitolea, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser amewaapisha wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani (Peace Corps Volunteers) wapatao 51 ili kuanza huduma yao ya miaka miwili. Wafanyakazi hawa wa kujitolea wa Kimarekani watafanya kazi katika sekta ya elimu. Mwaka uliopita katika Programu ya Elimu, wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps 110 walifundisha katika shule za sekondari 108 katika mikoa 22 kwenye zaidi ya wilaya 30 nchini Tanzania na kuwafikia takriban wanafunzi 36,000. Hawa wafanyakazi wa kujitolea 51 wanaungana na wengine 195 ambao tayari wako nchini wakifanya kazi katika elimu ya sekondari (hisabati, sayansi na kiingereza), kukuza sekta ya afya, na elimu ya mazingira.

Mheshimiwa Salum S. Salum, Afisa Elimu Mkuu, aliiwakilisha wizara ya elimu katika hafla ya uapisho. Hafla hii ilihudhuriwa pia na wafanyakazi wengine wa kujitolea wanaoendelea kuhudumu na wale waliomaliza muda wao pamoja na maafisa kutoka taasisi wabia.

Mbali na kufundisha madarasani nchini kote, wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps hushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii. Shughuli hizi ni kama kusaidia kuboresha maktaba za shule, kuandaa programu za kukuza uelewa wa VVU/UKIMWI, na kukuza stadi za maisha za wanafunzi. Wafanyakazi wa kujitolea walioapishwa leo, watapangiwa kufanya kazi katika wilaya zifuatazo nchini kote: Karatu, Kongwa, Chamwino, Mufindi, Iringa Rural, Hai, Rungwe, Lushoto, Wete, Nzega, Sumbawanga, Same, Ruangwa, Nachingwea, Hanang, Babati, Kiteto, Busokelo, Kyela, Chunya, Mbarali, Masasi, Newala, Mtwara rural, Mbinga, Morogoro Manispaa, Shinyanga, Kishapu, Maswa, Wanging’ombe, Singida, Njombe, Nzega na Lushoto.

"Wiki hii inaadhimisha miaka 55 ya kupitishwa kwa sheria ya Peace Corps, ambayo ilianzisha rasmi taasisi ya Peace Corps mwaka 1961. Kuwaapisha hawa wafanyakazi wa kujitolea katika maadhimisho haya maalum ni ishara ya kielelezo muhimu ya ushirikiano kati ya watu-kwa-watu ambao Peace Corps inahamasisha nchini Tanzania,” alisema Kaimu Balozi wa Marekani Virginia Blaser.

Zaidi ya Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps wapatao 2,000 wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1962. Peace Corps hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Marekani wanao fanyakazi katika jamii katika nyanja za elimu ya sekondari (wakifundisha hisabati, sayansi na teknolojia ya mawasilianoa), afya na elimu ya mazingira.

Peace Corps ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 7,000 katika zaidi ya nchi 70 duniani. Kwa miaka 50, Peace Corps imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini. Peace Corps ina dhamira ya kukuza amani na urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu yafuatayo:

• Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani watakaochangia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi itakayohitaji wafanyakazi hao;

• Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu katika jamii zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea;

• Kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na watu wake.

Zaidi ya Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps wapatao 2,000 wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1962. Peace Corps hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Marekani wanao fanyakazi katika jamii katika Nyanja za elimu ya sekondari (wakifundisha hisabati, sayansi na teknolojia ya mawasilianoa), afya na elimu ya mazingira.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: