Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dr.Leonard Subi (kushoto) akizindua Kondom mpya ya Zana inayotolewa na Serikali bure kwa wananchi kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi.
Kondom ya Zana ni mbadala wa kondom iliyokuwa ikitolewa pia bure na serikali na kusambazwa na Bohari ya Dawa nchini MSD ambapo kondom hiyo haikuwa na jina, rangi na kifungashio chenye kuvutia hali ambayo ilisababisha wananchi kudhania kwamba haina ubora jambo ambalo hata hivyo halikuwa sahihi kwani ilikuwa na ubora kama aina nyingine za kondom.
Uzinduzi wa Zana Kondom mkoani Mwanza
Waelimisha rika wakiwa kenye picha ya pamoja na mgeni rsami, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dr.Leonard Subi (mwenye suti).
Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro, amesema kumekuwa na dhana potofu kwa wananchi kuhusu kondom zinazotolewa bure na serikali kwamba hazina ubora jambo ambalo siyo sahihi ambapo amewahahikikishia kwamba kondom ya Zana ina ubora wa hali ya juu hivyo ni vyema wakazingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondom hiyo ili kuondokana na magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dr.Leonard Subi, amebainisha kwamba serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuwahudumia wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi hivyo ni vyema wakazingatia matumizi ya kondom ili kujikinga na maambukizi hayo.
Amesema ili kuondokana na matumizi hayo ya fedha, Serikali inawahimiza wananchi kuzingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondom, ili kuondokana na maambukizi ya virusi hivyo pamoja na maambukizi mengine ya magonjwa zinaa ikiwemo kaswende.
Dr.Subi ameyasema hayo hii leo kwenye uzinduzi wa kondom mpya ya Zana uliofanyika mkoani Mwanza, ambayo itakuwa ikisambazwa bure kwa wananchi na serikali ili kusaidia wananchi kuondokana na magonjwa ya zinaa pamoja na kimba zisizotarajiwa.
Amesema ni vyema wananchi wakaendelea kuhimizwa kuwa na matumizi sahihi na endelevu ya kondom ya Zana, hatua itakayosaidia kupunga ongezeko la waathirika wa magonjwa ya zinaa ikiwemo virusi vya Ukimwi na hivyo kuipunguzia serikali matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya kuwahudumia wenye maambukizi hayo.
Naye Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro, amesema kumekuwa na dhana potofu kwa wananchi kuhusu kondom zinazotolewa bure na serikali kwamba hazina ubora jambo ambalo siyo sahihi ambapo amewahahikikishia kwamba kondom ya Zana ina ubora wa hali ya juu hivyo ni vyema wakazingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondom hiyo ili kuondokana na magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa.
Uzinduzi wa kondom mpya ya Zana inayotolewa bure na serikali kwa wananchi, ulifanyika Kitaifa Agosti 30,2016 mkoani Mbeya ambapo kwa mkoa wa Mwanza umefanyika hii leo Jijini Mwanza ambapo wahamasishaji rika watakuwa wakipita mitaani kuwahamasisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya kondom hiyo na baadae uzinduzi kama huo utaendelea katika mikoa mingine nchini lengo likiwa ni kuwahamasisha wananchi kutumia kondom hiyo ili kusaidia mapambano dhidi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo virusi vya Ukimwi na mimba zisizotarajiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: