Kaimu katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja akimkabidhi bendera mshiriki wa mashindano ya walemavu ya Paralympiki Ignas Madumla akiwa na kiongozi wa msafara Tuma Dandi walioondoka leo mapema asubuhi kuelekea Nchini Brazil kwenye mashindano ya Olimpiki.
Mwanariadha
wa Tanzania, Ignas Madumla anayekwenda kushiriki mashindano ya Olimpiki
kwa walemavu, PARA LYMPIKI, yatakayofanyika jijini RIO DE JANAIRO, nchini
BRAZIL ameahidi kurejea na medali
Akizungumza baada ya
kukabidhi bendera ya taifa kwa mwanariadha huyo, kaimu katibu mkuu wa
baraza la michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja amemtaka mwanaridha huyo
kucheza kwa bidii ili arudi na medali.
Kwa upande
wao, mwanariadhi Ignas Madumla, na kiongozi wa msafara, Tuma Dandi
wamesema wamejiandaa vyema kuibuka na ushindi katika mashindano hayo.
Madumla
atashiriki katika mchezo wa kurusha kisahani na tufe.mashindano ya
PARALYMPIKI yanafanyika baada ya mshindano ya olympiki kumalizika huku
wawakilisha wa watanzania wakirejea na mikono mitupu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: