Na Mathias Canal, Dodoma

Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya wananchi (FDC)-CHISALU amekalia kuti kavu mara baada ya kubainika kuwa ameruhusu udahili wa wanafunzi wanaosoma fani ya utaalamu wa Kilimo na Mifugo ilihali chuo hicho ni maalumu kwa ajili ya mafunzo ya utaalamu wa Maendeleo ya jamii (Community Development).

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri amemsimamisha kazi Mkuu huyo kutokana na kupokea malalamiko ya baadhi ya wanafunzi chuoni hapo ambapo malalaniko yao yamekuwa na hoja za msingi zilizopelekea kuibuka kwa kadhia mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho.

Katika kutaka kubaini udhaifu unaohusu utendaji wa uongozi wa chuo hicho Dc Shekimweri alisikiliza hoja za wanafunzi chuoni hapo ambapo walitaka kujua sababu zinazopelekea wao kufanya mtihani unaoandaliwa na Chuo cha Ufundi VETA ilihali mtaala wao sio wa VETA.

Mbali na kadhia hiyo wanafunzi hao wamehoji pia fani ya kilimo wanafunzi hao wanayosoma ya Kilimo na Mifugo ambayo haitakiwi kwa mujibu wa taratibu pia haina namba ya mtihani (Exam Code) hivyo ni kwa kiasi gani wanafunzi hao watahakikishiwa ajira kama maafisa Mifugo pindi wamalizapo masomo yao.

Dc Shekimweri alizuru Chuoni hapo kwa lengo la kutaka kujua hatma ya wanafunzi wa chuo hicho kufungwa pasina sababu ndipo alipobaini uongo uliotumiwa na Mkuu wa Chuo hicho kwa kudai kuwa chuo kimefungwa kwa sababu ya kujiandaa na mitihani ambapo hata hivyo mtihani huo unataraji kufanyika Oktoba 10, 2016.

Mkuu wa chuo hicho alieleza kuwa chuo hicho kitafungwa hadi Tarehe 9/10/2016 siku moja kabla ya kufanyika kwa mitihani ambapo janja hiyo ilibainiwa na Mkuu wa Chuo kwa kudanganywa ratiba ya mtihani huo ambayo inaonyesha kuwa tarehe 26/09/2016 ndipo ambapo mtihani huo unataraji kuanza.

Hata hivyo Mkuu huyo wa chuo hicho amefunga chuo hicho pasina kushirikisha Bodi ya Chuo ambapo pia alihoji sababu za kudanganywa kufungwa chuo hicho bila maamuzi ya kusitisha kufanyika kwa mitihani ambapo ratiba yake imekwisha tolewa jambo ambalo lilimuacha mdomo wazi Mkuu huyo wa Chuo hicho.

Kutokana na kadhia hizo Dc Shekimweri amemsimamisha kazi Mkuu wa chuo hicho kwa kutumia uongo wakati wa kujitetea na kushindwa kitekeleza majukumu yake kikamilifu ikiwemo kutoitisha vikao vya Bodi, Kutosikiliza kero za wanafunzi hata alipojulishwa kwa maandishi na wanafunzi hao, kufunga chuo kwa dharula ilihali tatiba ya mtihani inaendelea na kuwashauri vibaya wanafunzi kuhusu hatima yao kutokana na mkanganyiko wa mtaala.

Dc Shekimweri alisema kuwa serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inahubiri zaidi uwajibikaji hivyo maamuzi hayo yanatuma salamu ili mamlaka ya uteuzi ifuatilie na kushughulikia tuhuma dhidi yake na kuchukua stahiki za kisheria.

Mkuu huyo wa Wilaya amesitisha Bodi ya chuo na kumtaka mwenye mamlaka nanuteuzi wa Bodi aivunje Bodi hiyo kwa kushindwa kukutana hata mara moja tangu bodi hiyo ilipoanzishwa Mwaka 2013hivyo kushindwa kitafsiri na kusimamia Dira kwenye mpango mkakati (Strategic Plan) pia kutokuwa na kalenda ya mwaka wa taaluma.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya pia alihoji pasina kupatiwa majibu kuhusu uidhinishwaji wa mpango wa bajeti wa chuo kuhusu anayeufanya ilihali Bodi haikutani kwa ajili ya vikao.

Dc Shekimweri alienda mbali zaidi kwa kutaka kujua vipi vipaombele vya chuo, mabadilko na mitaala, mafanikio na changamoto za chuo vinajadiliwa na kufikiwa maamuzi na watu gani iwapo Bodi haikutani kujadili.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya ya Mpwapwa alisema Changamoto za mitaala, Udahili na mtihani pamoja na vyeti vya kuhitimu litafanyiwa kazi kwenye Mamlaka husika (VETA) na Wizara ya Maendeleo ya Jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: