Na Anthony John, Globu ya Jamii

Mkuu wa Mkoa wa Dar as salaam, Mhe. Paul Makonda amewataka Watanzania kushiriki katika zoezi la kucheki afya zao litakalo fanyika Siku ya jumamosi katika eneo la Mnazi Mmoja kuanzia Saa mbili Asubuhi.

Pia amewataka wakazi wote wa mkoa wa Dar es Salaam kushiriki katika kucheki afya zao kwani wale wote watakao gundulika na matatizo mbali mbali watapata huduma za Papo hapo kwa madaktari bigwa hao kutoka katika hospitali mbali mbali

"Napenda kuchukua nafasi hii kuwaambia wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam tarehe 24 hadi 25 kutakuwa na zoezi la kucheki Afya zetu litakalo fanyika maeneo ya mnazi mmoja,kutakuwa na madaktari bigwa kutoka hospitali mbali mbali na kupata majibu sahihi Siku hiyo hiyo," amesema Makonda

Aidha Mganga Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Azizi Msuya amewataka wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kutokudharau magonjwa Madogo Madogo ambayo hayajapewa kipaumbele kwa hayo ni hatari zaidi ya yale magonjwa makubwa yanayo julikana.

"Tukiwa na tabia ya kufanya zoezi kama hili wengi watapata Hauweni ya matatizo Yao kwani watanzania wengi huwa na matatizo ya kiafya lakini wanashidwa kujua Afya zao,"amesema Azizi msuya
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: