Jumla ya shilingi milioni 187 zimepatikana kupitia mchezo wa kirafiki baina ya Wabunge Mashabiki wa Yanga na Simba kwa ajili ya kuwachangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

Mchezo huo ambao ulichezewa leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga wametoka kifua mbele kwa kufunga mabao matano kwa mbili. Yanga 5-2 Simba.

Akizungumza Waziri Mkuu Majaliwa mara baada ya kumalizika kwa mpambano huo, aliwashukuru wabunge na watu wote waliojitokeza kuiunga mkono kampeni hiyo iliweza kuleta matunda hayo.
Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja ambaye ni shabiki wa timu ya Simba akizungumza mara baada ya mechi kumalizika.
Waziri Mkuu Majaliwa akiwakabidhi kombe mashabiki wa timu ya Yanga ambao waliweza kushinda kwa bao 5-2.
Waziri Mkuu Majaliwa akiwagawia Medali.
Shangwe na vigeregere vilitawala uwanjani hapo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndungai akitoa shukrani kwa wabunge na ndugu, jamaa na marafiki walioweza kujitokeza.
Waziri Mkuu Majaliwa akiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kushuhudia mpambano wa Wabunge Mashabiki wa Yanga na Mashabiki wa Simba.
Waziri Mkuu Majaliwa akikagua Wabunge mashabiki wa Yanga na Simba.
Wabunge Mashabiki wa Simba.
Wabunge Mashabiki wa Yanga.
Wakiimba wimbo wa Taifa.
Mtanange ukiendelea... Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete akimiliki mpira wakati wa mchezo wao wa Bonanza uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mchezaji wa Wabunge wa Yanga, Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akimenyana na Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja wakati wa mchezo wao wa Bonanza uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mchezaji wa Wabunge wa Yanga, Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akimpiga chenga kipa wa wabunge wa Simba, Jaku Hashim wakati wa mchezo wao wa Bonanza uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: