Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
Wanawake wa Jimbo la Segerea wakiwa kwenye semina ya ujasiriamali ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Wanawake wa Jimbo la Segerea wakiwa kwenye semina ya ujasiriamali ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Mama mjasiriamali akichangia mada katika semina hiyo, huku Wanawake wajasiriamali wa Jimbo la Segerea wakisikiliza kwa makini wakufunzi waliokuwa wakizungumza kwenye semina ya ujasiriamali ya kuwainua kiuchumi wanawake. PICHA ZOTE na SHUNDA BLOG.
Mwenyekiti wa Vikundi vya Wanawake Wajasiriamali wa Jimbo la Segerea, Salma Fumbwe, akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (kushoto) katika semina ya ujasiriamali ya wanawake iliyofanyika ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima,jijini Dar es Salaam,leo. Kauli Mbiu ni Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi”.
---
Na Elisa Shunda

WANAWAKE washauriwa kutenganisha fedha ya msingi wa biashara na fedha ya matumizi mbalimbali ya nyumbani ili kuboresha na kusonga mbele kiuchumi tofauti na wakichanganya watakuwa wanadumaza biashara zao na matokeo yake kupata hasara inayopelekea kusimamisha biashara anayoifanya.

Hayo yamezungumzwa na wakufunzi mbalimbali waliokuwa wakitoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake kwenye semina yenye ujumbe wa kauli mbiu ya Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza kwenye semina hiyo mbunge wa jimbo hilo, Bonnah Kaluwa,alisema kuwa ameamua kuandaa semina ya ujasiriamali ya wanawake kwa ajili ya kuwapatia elimu mbambali za ujasiriamali pamoja na elimu ya utunzaji wa fedha za biashara kwenye sehemu yenye uhakika pasipokuwa na shaka wala wizi kwa kuwaletea benki ya Equity na Mfuko wa hifadhi ya Jamii ya PPF ambao watawasaidia kuwahifadhia fedha zao pamoja na kuwapatia bima ya afya na fao la kustaafu endapo watakidhi vigezo.

“Wakinamama nimefurahi kwa jinsi mlivyojitokeza kwenye semina hii natumaini tukimaliza hapa kila mmoja wetu atakuwa amepata elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya ujasiriamali likiwemo la kutofautisha fedha ya matumizi ya nyumbani na fedha ya biashara kwa kuwa ukipata elimu ya kutenganisha vitu hivyo utaendelea kwenye biashara yako huwezi kutoa fedha ya biashara kununua chakula au kumsomesha mtoto lazima utayumba hivyo ni bora kila mtu ategeshe sikio lake vizuri kusikiliza elimu itakayotolewa hapa ambayo itatufumbua kutofautisha masuala ya nyumbani na biashara ambayo itatusaidia sana kufikia kwenye malengo yetu” Alisema Kaluwa

Semina hiyo ya ujasiriliamali kwa wanawake wa jimbo la Segerea itawezesha kuwapatia elimu ya utunzaji wa fedha akinamama zaidi ya 500 ambao wapo kwa kanda mbili ambapo mkutano huu wa mwanzo ulifanyika kwenye jimbo hilo kwa kanda ya A ambapo baadae kanda B nao watapatiwa elimu hiyo kupitia ufadhili wa benki ya Equity na Mfuko wa Hifadhi ya jamii kushirikiana na ofisi ya jimbo la Segerea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: