Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasilini Mkoani Kagera wakitokea nchini Uganda kushiriki mashindano ya CECAFA kwa wanawake ambapo wameibuka mabingwa kwa mwaka 2016.
Mabingwa wapya wa Kombe la Chalenji la CECAFA, timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens, mara baada ya kutua hapa Mjini Bukoba leo Asubuhi wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera , Meja Jenerali mstaafu Salum Kujuu na kuwapongeza kwa Ushindi huo mkubwa walioupata kwa kuifunga Timu ya Kenye bao 2-1.

Timu hii inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kesho Septemba 22, 2016 saa 7.00 mchana kwa ndege ya FastJet ikitokea Mwanza.

Mara baada ya kutua, itakwenda moja kwa moja kwenye Hoteli ya Coartyard iliyoko Sea View, Upanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ambako watakuwako viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wale wa Serikali akiwamo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi.
Ni baada ya kuwaunga Timu ya Kenya bao 2-1.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu(kushoto)  akipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa katibu wa Chama cha Mpira mkoani  Kagera Bw. Salum Chama mara baada ya Mabingwa wa CECAFA kwa wanawake  Kilimanjaro Queens kuwasili kutoka Nchini Uganda katikati ni Mwenyekiti  wa Soka la wanawake Amina Karuma.
Mc Baraka akiinua juu kikombe cha Ubingwa wa CECAFA kwa wanawake alichokipokea kutoka kwa Nahodha wa Kilimanjaro Queens Sophia Mwasikili pichani (kulia) katika kuwapongeza kwa Ushindi. Picha kwa hisani ya Bukobawadau Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: