Na Emmanuel S. Seni.

Tangu uchaguzi mkuu ufanyike mpaka sasa, bado hatujawa na sera yenye dira pevu na yenye muda akisi kulingana na Ilani ya uchaguzi mkuu inayoweza kutuongoza kwa mageuzi ya viwanda hapa nchini, hasa katika kipindi cha mwaka 2016-2020. Kama jinsi inavyo someka hapa chini.

1. Kustawisha na kuimarisha sekta kuu mtambuka zenye mahusiano ya karibu na ukuaji wa viwanda, kuwa mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa huduma, bidhaa na ajira endelevu.

2. Kuandaa mpango kabambe (Master Plan) kwa matumizi tengefu ya ardhi itakayofanyiwa upimaji kwa maendeleo ya viwanda katika ngazi ya kanda, mikoa na kila wilaya.

3. Kujenga viwanda vipya vya kusindika mazao ya misitu, kilimo, uvuvi na ufugaji. Hivi inahitajika takwimu, mipango na kanda maalumu za kiuwekezaji kwa kuingia mikataba ya kuleta technologia ya kutengeneza bidhaa badala ya kuleta bidhaa.

4. Kutoa kipaumbele na vishawishi maalum kwa viwanda vya kuendeleza kilimo. Kwa mfano, kuendeleza viwanda vya pembejeo, mbolea, pia viwanda vya mbegu bora na madawa ya kilimo.

5. Kukuza na kuendeleza miundombinu yote ya usafirishaji pamoja na usambazaji wa huduma za nishati ili kuleta msisimko wa ukuaji wa sekta ya viwanda.

6. Kukuza na kuendeleza fani mbalimbali za kilimo na uzalishaji mali katika vyuo vya elimu ya juu na mafunzo ya ufundi.

7. Kufufua na kuongeza viwanda vyetu vya nguo au mavazi ili tuweze kuzalisha kiwango kikubwa cha pamba na ngozi inayozalishwa Tanzania.

8. Kuimarisha na kukuza usindikaji wa mazao ya nafaka, mafuta, korosho, katani, kahawa, tumbaku na chai ili kuhakikisha ongezeko kubwa la thamani katika mazao haya na ongezeko kubwa la bidhaa zinazotokana na mazao haya.

9. Kuanzisha na kuendeleza Benki ya ukuzaji wa viwanda pamoja na ukuzaji na ustawishaji ushirika wa viwanda na biashara.

10. Ukuzaji na ustawishaji wa shirika la kiutafiti na uendelezaji wa sekta ya viwanda na biashara nchini.

11. Kuwepo kwa soko kubwa la viwanda vya ndani ya nchi kwa ajili ya ununuzi wa malighafi mbalimbali za kilimo, uvuvi, ufugaji, misitu, maliasili n.k.

12. Vijana wengi na wanawake kupata ajira katika viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vitakavyojengwa na kuendelezwa.

13. Kuongezeka kwa mauzo ya nje ya nchi na kupungua uingizwaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kwa sera maalumu ya kifedha na masoko.

14. Kuongeza huduma za makazi bora, yenye huduma zote muhimu za kijamii, kwa watumishi wa viwandani.

15. Kuboresha na kuongeza huduma za mifuko ya hifadhi kwa jamii kama afya na pension, ikiwa pamoja na vyama vya wafanyakazi, vikundi vya akiba na mikopo.

16. Kufanya ushawishi wa ushirikishwaji wa wadau mbalimbali, kuweza kujitokeza katika uwekezaji, ukuzaji na ustawishaji wa sekta ya viwanda na biashara ili kuweza kupanua soko la ndani na nje ya nchi.

N.B: Baadhi ya Maoni Yanatokea Katika Sera za Ilani ya Uchaguzi, Chadema 2015.
Emmanuel S. Seni. Simu: 0787220120.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: