Nianze kukupa hongera na pole ya kazi ngumu na nzito ya ujenzi wa Taifa letu. Naelewa dhamira safi iliyopo ndani ya moyo wako ya kutaka kulifanya Taifa letu liwe na maendeleo.
Leo mimi nimeona niandike barua hii ya kuomba uteuzi wa Ras Kagera. Nafahamu sana kuwa si jambo la kawaida mtu kuomba uteuzi,lakini naomba nikukumbushe kuwa Mungu alipouliza nimtume nani akakomboe watu wangu,Yesu alisimama na kusema nitume mimi,hivyo basi pamoja na kwamba hujauliza binafsi nimeamua kujitokeza mapema kuomba nafasi hiyo.
Dhamira yangu imenituma,hali na moyo wangu unahitaji hiyo kazi,na nitakwenda kuhifanya kwa uadilifu mkubwa na uaminifu wa hali ya juu.
Nina sifa na vigezo vyote vya kufanya hiyo kazi na kwa hakika nitarejesha matumaini yako kwetu sisi wateule wako,maana nafahamu inaumiza sana kuona watu uliowaamini kutoka miongoni mwa Watanzania milioni 40 kwenda kufanya wizi kama huu uliotokea Kagera.
Nafahamu pia Mhe Rais wangu, una vyombo vyote vya kuweza kupata wasifu wangu, nina dhamira ya dhati na safi kutumikia nchi yangu,.hivyo nakuomba kabla ya birthday yako tarehe 29 mwezi Oktoba, naomba niwe tayari Kagera ili nikasimamie ile misaada iwafikie waathirika ambao wewe unawapigania wapate misaada hiyo.
Mhe Rais niwie radhi,wala sikufundishi kazi,najaribu tu kuomba,na nipo tayari kwa usahili wakati wowote ukinihitaji.Binafsi napenda sana kufanya kazi na wewe,dhamira safi uliyonayo ndio inayonisukuma.
Nina elimu ya chuo kikuu,nina miaka 31,ni mtanzania, naishi Morogoro. Nina familia.
Nakushukuru sana,najua barua yangu itafanyiwa kazi itakapofika kwenye meza yako tukufu.
Wasalaam,
Edward Clement Kyungu
Mahenge/Ulanga
MOROGORO.
28/09/2016
Toa Maoni Yako:
0 comments: