Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeanzisha na kuzindua namba maalumu kwa watanzania kuchangia ili kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mnamo tarehe 10 Septemba 2016 majira ya mchana huko Bukoba mkoani kagera. Watu 17 wamepoteza maisha na kuacha mamia wakiwa hawana makazi kufuatia tetemeko hilo.

Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Huduma za jamii Hawa Bayumi alisema, “Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na wanafamilia kutokana na tetemeko hili pia limewaacha mamia wakiwa hawana makazi. Leo tunaungana na wakazi wa Kagera katika janga hili kwa kutoa mchango kwa waathirika wa tetemeko na kuwaomba watanzania wote kuungana nasi kwa kuchangia kupitia namba maalumu 155990 itakayotumika kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika wa janga hili wanaohitaji msaada wa haraka.

Jinsi ya kuchangia ni rahisi,

unapiga *150*60# kuingia kwenye airtel money

unachagua 5 yaani lipa bili kwa Airtel Money,

kisha unachagua 4 andika jina la biashara ambapo utaandika 155990,

Kisha ingiza kiasi cha fedha unachotaka kuchangia

Weka kumbukumbu namba ambayo ni jina lako

Kisha malizia kwa kuweka namba ya siri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: