Msanii
wa kimataifa toka Nigeria Ayodeji Balogun(Wizkid) akitumbuiza katika
tamasha la Tigo Fiesta 2016 liliofanyika hapo jana Jijini Mwanza katika
viwanja vya CCM Kirumba
Baadhi
ya waandishi wa Habari wakichukua matukio katika tamasha la Tigo Fiesta
2016 wakazi msanii wa kimataifa toka Naijeria Wizkid akitumbuiza katika
viwanja vya CCM kirumba usiku wa jana.
Baadhi
ya wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia wakati burudani mbalimbali
zikitolewa na wasanii waliotikisa jukwaaa la Tigo Fiesta 2016 hapo usiku
wa jana katika viwanja vya CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mkali wa singeli ManFongo na Shilole wakilivamia jukwaa la Tigo Fiesta 2016 katika tamasha hilo kubwa liliofanyika usiku wa jana jijini Mwanza na kukutanisha wasanii nguli katika muziki wa kizazi kipya na Msanii wa kimataifa toka Nijeria Wizkid
Umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza wakitoa shangwe wakati burudani mbalimbali zikiendelea katika Tamasha la Tigo Fiesta 2016 viwanja vya CCM Kirumba hapo usiku wa jana.
Alikiba alikuwa kivutio kwa mashabiki wengi mara baada ya kufanya suprize na kutoa burudani ya kukata na shoka huku mashabiki zake wakifuatisha nyimbo zake moja baada ya nyingine katika Tamasha la Tigo Fiesta 2016 katika viwanja vya Kirumba Jijini Mwanza
Benpol akilishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2016 lilifnayika jana katika viwanja vya CCM kirumba Jijini Mwanza.
Msanii wa kizazi kipya Dayna Nyange akitumbuiza umati uliohudhuria Tamasha la Tigo Fiesta 2016 jijini Mwanza hapo usiku wa jana.
Mkali wa Singeli anayetamba na nyimbo yake "HAINAGA USHEMEJi" akitumbuiza jukwaa la Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza.
Aika na Nahreel (Navykenzo) nao walifanikiwa kuteka jukwaa la Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza
Wasanii toka kikundi cha TipTop connections Tundaman na Madee Ali wakitumbuiza mashabiki katika jukwaa la Tigo Fiesta 2016 katika viwanja vya CCM kirumba hapo usiku wa jana.
Weusi wakilishambulia vilivyo jukwaaa la Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza hapo usiku wa jana.


Toa Maoni Yako:
0 comments: