Baba mmoja alikuwa na wake wanne, Alimpenda sana mke wake wa nne na alitumia gharama kubwa kwaajii yake na kumpa matunzo bora.

Pia alimpenda mke wake wa tatu na siku zote alipenda kuwaonyesha marafiki zake mke huyu wa tatu kwakuwa alikuwa mrembo kwelikweli.

Hata hivyo alikuwa na hofu kwamba huenda mke huyu anaweza msaliti aende kwa mtu mwingine kati ya hao rafiki zake.

Pia alimpenda mke wake wa pili kwakuwa kila alipokabiliwa na matatizo mke huyu alikuwa faraja na msaada mkubwa katika kumshauri.

Hata hivyo, huyu baba hakuwa na upendo kabisa na mke wake wa kwanza japo mke huyu alimpenda sana mume wake na alikuwa mwaminifu sana kwake.

Siku moja yule baba aliumwa sana na alijua kwamba hana muda mrefu wa kuishi.

Akajiambia mwenyewe "Kwakuwa nina wake wanne nitachagua mke mmoja ninayempenda sana tufe wote ili tukaishi tena pamoja peponi"

Akamwomba mke wa nne afanye chochote ili afe pamoja nae. Mkewe akamjibu huku akiondoka "Hapana!" .

Ikabidi amuite mke wake wa tatu akamwambia atumie njia yoyote ile ili wafe wote, mkewe akamjibu akamwambia "Maisha ni mazuri sana duniani, we kufa tu mi niko tayari kuolewa tena na mume mwingine".

Akaamua kumuita mke wake wa pili akamwambia vilevile kama alivyowambia wake zake wawili. Mkewe akamwambia " Pole sana, kwa hili sitaweza kukusaidia ila nitakusindikiza mpaka makaburini utakapozikwa."

Matumaini yake yakapotea, na sasa akaanza kuhisi baridi. Hapo akasikia sauti kwa mbali kutoka kwa mke wake wa kwanza:-

"Mimi Niko tayari kuondoka na wewe. Nitakufuata popote utakapokwenda."

Yule baba kwa taabu akafumbua macho akatazama, akamwona mke wake wa kwanza amedhoofu sana kama mtu mwenye utapiamlo.

Kwa huzuni nyingi, yule baba akasema, "Laiti ningejua kuwa wewe ndiye mwenye mapenzi ya dhati, ningekutunza na kukugharamiakia kadri ya uwezo wangu."Lakini sasa nimechelewa siwezi kufanya hivyo, najuta kwa kutokukujali!"

FUNDISHO:-
Maisha tunayoishi ni kama tuna wake wanne.

4⃣ Mke wa nne ni mwili wako, tunatumia gharama kubwa kuupendezesha na kuutunza uonekane wa kuvutia lakini hatuendi nao popote wakati wa kufa, unayarudia mavumbi yake.

3⃣ Mke wa tatu ni malizetu, hadhi na utajiri. Japo tunahangaika kuvitafuta, tunapokufa hatuendi navyo popote..wanabaki navyo wengine.

2⃣ Mke wa pili ni familia zetu na marafiki. Hata wakitupenda na kuwa karibu nasi kiasi gani, hawawezi kufa na sisi, watakachoweza kufanya ni kutusindikiza hadi makaburini na sio zaidi ya hapo!!!

1⃣ Mke wa kwanza ni Maisha yetu ya kiroho yenye manufaa makubwa ya uzima wa milele, ambao katika harakati zetu za maisha na azma yetu ya kutafuta utajiri wa mali na raha za dunia tumeutupa mbali.

Mungu akusaidie kujali na kushibisha Roho❤ yako zaidi ya vingine vyoote‼

✝MITHALI 4:23 - "Linda moyo (roho) y/wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokazo chemchemi za UZIMA

👫Mwanadamu ni *roho yenye nafsi inayokaa ndani ya mwili
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: