TUME ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora nchini, imekitaka chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha kutumia neno “udiktekta” kwenye harakati za kisiasa, kwani Tanzania ni nchi yenye kuzingatia misingi ya kidemokrasia na yenye kuheshimu utawala wa kisheria.
Aidha, imekitaka chama hicho kusitisha maandamano waliyopanga kufanyika Septemba mosi, hadi mahakama itakapotoa tafsiri ya uhalali wa zuio la mikutano ya kisiasa lililotolewa na Polisi Juni saba, mwaka huu.
Pendekezo hilo la tume, limetolewa kwa kuzingatia kuwa, CHADEMA imeshafungua mashauri mawili kwenye Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam na Mwanza, kuomba mahakama kutoa tafsiri kuhusu zuio la mikutano hiyo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: